Kutoka Kushoto ni Mratibu wa Asasi ya Mwado tawila la Kiteto Bi. Paulina Kiria Akimkabidhi Vifaa Hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona Mbele ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmshauri ya Kiteto.
Kutoka Kushoto ni Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kiteto Akielezea Jambo Wakati wa Makabidhiano Hayo Karibu na Ukumbi wa Kitengo cha Ugavi Mbele ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmshauri ya Kiteto.
Aliyevaa Gauni Refu la Mistari ni Mratibu wa MWADO Tawi la Kiteto Bi. Paulina Kiria na Kushoto Kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona
----------------------------- HABARI KAMILI -----------------------------
Asasi hiyo yenye makao makuu yake Arusha yenye tawi lake Kiteto na Balaza la Wanawake wa Kifugaji (Pastoral Women Council) kwa kushirikiana na wafadhili wao wa Shirika la COMIC RELIEF la Uingereza wametoa msaada huo leo asubuhi, ambapo vifaa kinga hivyo ni Ndoo kubwa (DIABA) 40, Thermal Scanner 2 kwa ajili ya kupimia hali joto kwa binadamu na Sanitizer galoni 30 vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Tshs. 1,720,000/=.
Mratibu wa Asasi ya MWADO tawi la Kiteto Bi. Paulina Kiria amesema tunawasilisha msaada huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ili kuongeza nguvu kwa Serikali katika kusaidia kupambana na maambuzi ya COVID-19 katika sekta ya elimu hususani sehemu ya shule za sekondari na shule za msingi Wilayani Kiteto.
Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona akiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo amesema anawashukuru sana wote waliojitolea vifaa hivi kwa upendo wao kwa wanafunzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwani bado tunatakiwa kuendelea kujikinga kwani tatizo bado lipo miongoni mwetu hivyo vifaa hivi ni muhimu na vitasaidia sana wanafunzi wetu kujikinga na Covid-19.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa