• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Madiwani Watakiwa Kushiriki Katika Ukusanyaji wa Mapato

Imetumwa : March 1st, 2019

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel akizungumza wakati akifunga kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya halmashauri kwa mwaka 2019/2020.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel akiongoza kikao .

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto akitoa ufafanuzi kuhusiana na michango ya Wahe. Madiwani kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kiteto Ndg. Mohamed Kiondo akizungumza wakati wa kikao .

Wahe. madiwani wakichangia kuhusiana na bajeti iliyowasilishwa .

Wahe. madiwani wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa bajeti.Aliyesimama mbele (mwenye joho Jeusi )  ni kaimu Afisa mipango (W)  ambaye ndiye aliyewasilisha bajeti hiyo Ndg. Edga Kavenuke.

Wataalamu kutoka idara mbalimbali za halmashauri ya wilaya ya Kiteto wakiwa kikaoni.



........HABARI KAMILI.........


Madiwani  Watakiwa Kushiriki  Katika  Ukusanyaji wa Mapato


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mheshimiwa Lairumbe Mollel  amewataka waheshimiwa madiwani kushirikiana na wataalamu wa halmashauri katika ukusanyaji wa mapato,ili bajeti waliyoipitisha iweze kutekelezeka.Mhe. Lairumbe ameyasema hayo wakati wa kikao cha kupitisha bajeti ya halmashauri kwa mwaka 2019/2020.


Akizungumza  wakati akifunga kikao hicho Mhe. Mollel amesema kwamba fedha zilizopitishwa kwenye bajeti ziko kwenye makaratasi,ili zipatikane ni lazima ushirikiano uwepo.Akisisitiza kuhusu ushirikiano huo, Mhe Mollel amesema “Bajeti ni mapendekezo tu, uhalisia wake unatokana na ukusanyaji wa mapato.Ukusanyaji wa mapato ndio utatupa dira kwamba halmashauri yetu itaendaje.Sisi kama  madiwani kule kwenye kata zetu, tuhakikishe kwamba tunapamba  kudhibiti utoroshwaji wa mazao.Na tunasimamia vizuri ukusanyaji mapato.Usimamizi wa mapato sio wa Mkurugenzi ,wala sio wa wataalam pekee,kazi hiyo ni ya kwetu sisi zaidi kama wasimamizi wa halmashauri hii”.


Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kiteto ndugu Mohamed Kiondo ametilia mkazo kauli ya mwenyekiti wa halmashauri ambapo amewataka  waheshimiwa Madiwani kusaidia usimamizi  ukusanyaji mapato kwenye kata zao,ili miradi inayokusudiwa kutekelezwa kupitia bajeti hiyo iweze kutekelezeka.


Aidha ndugu Kiondo ameipongeza halmashauri kupitia mkurugenzi mtendaji wake ndugu Tamim H. Kambona kwa miradi yenye viwango, ambapo amesema kwamba wilaya ya Kiteto ndiyo inayoongoza mkoani Manyara kwa miradi yenye viwango.


Katika hatua nyingine diwani wa kata ya Kaloleni Mhe. Christopher Permeti amempongeza  Mkurugenzi mtendaji pamoja na wataalam wa halmashauri kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati  katika bajeti hiyo ambapo amesema kwamba mapendekezo yote waliyoyatoa  kwenye  vikao vya kamati yamefanyiwa kazi.

Kikao hicho cha baraza la madiwani ambacho ajenda yake kuu ilikuwa ni kupitisha bajeti, kilitanguliwa na vikao vya kamati za kudumu za halmashauri ambapo kamati zote zilipitia  na kujadili kwa kina na kutoa mapendekezo yake kuhusiana na bajeti hiyo. Kikao kilihitimishwa baada ya Wahe. madiwani wote kwa kauli moja kuridhia na  kupitisha  bajeti ya sh. 31,707,464,722.75, ambapo kati ya fedha hizo sh. 2,273,486,000/= zinatarajiwa kupatikana kupitia makusanyo kutoka katika vyanzo ya ndani ya Halmashauri.



.

........MWISHO.........







Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • JAMII YAASWA KUZINGATIA HAKI ZA WATOTO.

    June 16, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa