• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mafunzo ya Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Awamu ya Pili na Uwekazi Wazi wa Daftari la Wapiga Kura Yafanyika kwa Tahadhari ya Hali ya Juu Leo Tarehe 15.04.2020 Katika Ukumbi wa Community Centre.

Imetumwa : April 15th, 2020

Afisa Mwandikishaji Ngazi ya Jimbo Bw. Tamim H. Kambona ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Akifungua Mafunzo Hayo.


Mh. Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto Johakimu J. Mwakyolo Akisalimia na Kuanza Zoezi la Kuwaapisha Watendaji Wote wa Wilaya ya Kiteto 

Hapo juu ni washiriki wenyewe wa zoezi hili wakinawa mikono  kabla hajaingia ukumbini hapo.



Washiriki wa mafunzo haya kama wanavyoonekana mpenzi msomaji



------------------------------------------------------------    HABARI KAMILI    ------------------------------------------------------------




Katika mafunzo hayo mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw.Tamim H. Kambona alisisitiza washiriki wote kuwa na tahadhari ya ugonjwa wa Corona "Covid 19" kwa kufuata kanuni za kitabibu zinazotolewa na Serikali. hata hivyo Bw. Kambona aliongeza kuwa kila mtu awe makini kwa kusikiliza na kufanya mazoezi kwa vitendo kwa wingi ili kila mmoja akielewa vizuri itaongeza ufanisi wa uboreshaji wa daftari hili katika Halmashauri yetu.

Mafunzo haya ni ya siku moja tu, ambapo kesho kutwa tarehe 17.04.2020  tutaanza uboreshaji wa daftari hili kwa muda wa siku tatu hadi tarehe 19.04.2020 katika Kata zote 23 za Wilaya yetu ya Kiteto ambapo kila kata itakuwa na kituo kimoja chenye Mashine ya kuandikishia (BVR Kit) moja kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12 jioni.

Kwa kuzingatia hali ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona "Covid 19" kanuni zote za kiafya zilifuatwa katika hatua zote kwa kuwepo ndoo yenye maji safi yanayotiririka ya kunawia na vitakasio vya aina mbalimbali ambapo kila mtu anayeingia na kutoka lazima apitie hatua hizo, katika ukaaji pia zingatio la mita 1 hadi 2 ulizingatiwa ipasavyo na muhimu zaidi walitumia muda mchache kufanikisha haya ili kujikinga na ueneaji wa ugonjwa huu wa Corona "Covid 19".

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji imetoa matangazo ya kutosha kwa njia ya kubandika matangazo hayo kwenye mbao za matangazo Ofisi zote za Vijiji na Kata na maeneo mengine maarufu pia kutangaza kwa kutumia magari kwa Wilaya nzima katika kata zote kuhamasisha wananchi kufika vituo husika kuhakiki taarifa zao kwa muda na tarehe tajwa hapo juu ili kuweza kurekebisha taarifa zao kwa wale wenye mahitaji.

Pia unaweza kuhakiki taarifa zako kwa njia ya mtandao kupitia simu yoyote ya mkononi kwa namba *152*00#  kisha fuata maelekezo utakayokuwa unapewa lakini waweza ingia kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi yenyewe kwa anwani ya www.nec.go.tz inashauriwa pia ni vema mtu akatumia njia hii kuhakiki taarifa zao kupunguza mzunguko wa muhusiaka na kuweza kuzuia janga la Corona "Covid 19"

Katika zoezi hili suala la kuzingatia kanuni za kuzuia ueneaji wa Corona "Covid 19" utaendelea kwa kila kituo kuwepo kwa ndoo mbili moja ya maji ya kunawia na nyingine kukingia maji machafu ikiwemo na kitakasa mikono, pia kwa kila foleni itakayokuwepo basi umbali husika utazingatiwa.

Mwisho kila muhusika azingatie maelekezo yote atakayopewa na akafanye kazi kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu ili ufanisi uwe kwa asilimia mia moja.




Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • JAMII YAASWA KUZINGATIA HAKI ZA WATOTO.

    June 16, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa