• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wanawake Watakiwa Kutambua Nafasi Yao

Imetumwa : March 8th, 2019

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Emmanuel Mwagala ( aliyesimama) akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.Maadhimisho hayo kiwilaya yamefanyika katika kijiji cha Ngipa ,kata ya Engusero.

Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya,kaimu Mkurugenzi Mtendaji  pamoja na wananchi kutoka maeneo  na taasisi mbalimbali wilayani Kiteto wakipanda miti kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Afisa tarafa ya Kibaya Bi. Dhulfa Laizer  akiwasilisha hotuba  ya Mkuu wa wilaya ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.

Diwani wa kata ya Engusero Mhe. Solomoni Mbulunyuku akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.

Mmoja kati ya wajumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Kiteto ambaye pia ni diwani V/M Tarafa ya Kibaya  Mhe. Ngaisi akizungumzia mimba za utotoni wakati wa maadhimisho hayo.

Dkt. Mwanaidi Shabani kutoka hospitali ya wilaya ya Kiteto akizungumza kuhusu  uzazi  salama wakati wa maadhimisho hayo.

Wanawake kutoka maeneo mbalimbali  wilayani Kiteto wakiwa wamekusanyika katika maadhimisho hayo.

Wanawake wakicheza muziki  wakati wa maadhimisho hayo.

Vikundi vya wanawake vya ngoma za asili vikitumbuiza katika maadhimisho hayo.




................ HABARI KAMILI..........



Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri  ya wilaya ya Kiteto ndugu Emmanuel Mwagala amewataka wanawake wilayani Kiteto kutambua na kukaa kwenye nafasi yao sawasawa. Mwagala ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kiwilaya yamefanyika katika kijiji cha Ngipa kata ya Engusero .

Akizungumza wakati  akimkaribisha mgeni rasmi Mwagala amesema “ Mtoto akizaliwa mwalimu wake wa kwanza ni mama,ninyi wanawake mna nafasi kubwa  na umuhimu mkubwa sana katika maisha ya mwanadamu hapa duniani,lakini bado wengi wenu hamjatambua  umuhimu wenu na kuchukua nafasi yenu na kuifanyia kazi.Tambueni nafasi yenu muitendee haki.Ulimwengu ulishatambua umuhimu wenu katika jamii tangu zamani.Na ndio sababu muafrika wa kwanza msomi aliyeitwa daktari Agrey alifika mahali akasema kwamba ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii”

Mwagala amewataka wanawake kuachana na dhana zinazolenga  kumdhoofisha mwanamke na kumdhalilisha mwanamke .Hapa anasema “ Achaneni na nadharia ambayo ililetwa na watu wachache ambao walimtazama mwanamke kama chombo cha starehe, kiumbe dhaifu ambaye kila anachokifanya ni kwaajili ya kumpendeza na kumfurahisha mwanaume.Ondokeni huko, achaneni na hiyo dhana potofu , mna nguvu kubwa ambayo mkiamua kwa dhati kukaa kwenye nafasi yenu na mkaituia vizuri hiyo nguvu iliyomo ndani yenu mtaweza kufanya mambo makubwa sana”.

Kadhalika Mwagala amewataka wanawake  kusimama kidete  kuhakikisha kwamba watoto wakike wanakwenda shule  kama ilivyo kwa watoto wakiume.Mwagala amesema kwamba kwa miaka mingi mtoto wa kike amekuwa akitazamwa kama mtu wa kufanya kazi za nyumbani, na kitega uchumi cha wazazi,hali hiyo ya kumtazama kama kitega uchumi imesababisha watoto wa kike kuozeshwa wakiwa na umri mdogo ili wazazi wapate mahari, bila kujali kwamba kufanya hivyo kunawanyima  watoto wa kike haki ya kusoma, na kunakatisha malengo yao na hatimae kuharibu kabisa mustakabali wa maisha yao.

Naye Kaimu Afisa maendeleo ya jamii wilaya ndugu Steven Mafuru amesema kwamba siku ya wanawake duniani imewekwa kwa lengo la kuikumbusha jamii kutambua thamani na nafasi ya mwanamke katika jamii.Hivyo katika kuadhimisha siku hiyo ni vema jamii ikaendelea kuelimishwa na kukumbushwa  nafasi ya mwanamke katika jamii , mwanamke akipewa nafasi na fursa ana uwezo wa kufanya mambo makubwa.Atambuliwe, athaminiwe na aheshimiwe.

Katika hatua nyingine Umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi wilayani hapa wamewataka wanawake kutofumbia macho tabia na mienendo ambayo inachochea mimba za utotoni,badala yake wasimame kwa nguvu moja kukemea vitendo hivyo ili kutokomeza tatizo la mimba za utotoni ,tatizo ambalo katika miaka ya hivi karibuni limeendendelea kushika kasi.

Aidha Daktari Mwanaidi Shabani kutoka hospitali ya wilaya ya Kiteto amewataka wanawake kujitendea haki wakati wanapokuwa wajawazito kwa kuanza kliniki mara tu wanapohisi kwamba ni wajawazito, na wakati wa kujifungua unapofika waende kujifungulia katika vituo vya afya au hospitali,wasijifungulie majumbani  kwa sababu wakati wa kujifungua hatari ni nyingi sana, hivyo wanapojifungulia majumbani wanahatarisha maisha yao na ya watoto wao.

Katika maadhimisho hayo wanawake wa kijiji cha Ngipa wamewasilisha kero zao kwa mgeni rasmi ambapo kero hizo ni kukosa huduma ya maji katika maeneo ya karibu, hali ambayo inawalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji.Ukosefu wa zahanati katika kijiji chao,hivyo kulazimika kufuata huduma za matibabu katika makao makuu ya kata (Engusero)katika hili wamemuomba mgeni rasmi awasaidie jengo lao la zahanati ambalo limeshapauliwa limaliziwe li huduma za afya  ziweze kupatikana kijijini hapo.Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo bibi Dhulfa Laizer ameahidi kuzifikisha kero hizo kwa mkuu wa wilya ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Tarehe 8 Machi kila mwaka ni siku ya wanawake duniani, ambapo nchi zote wanachama wa umoja wa mataifa huadhimisha siku hiyo.Mwaka huu 2019  wilayani  Kiteto, maadhimisho hayo hayo yaliambatana na zoezi la upandaji miti  .





...........MWISHO............


Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • JAMII YAASWA KUZINGATIA HAKI ZA WATOTO.

    June 16, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa