• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

HALMASHAURI YATOA 50M KUMALIZIA ZAHANATI YA KIJIJI CHA ENGUSERO ENGINE

Imetumwa : March 19th, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kupitia mapato ya ndani kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 imetoa kiasi cha shilingi milioni 50 kwaajili ya umaliziaji wa  boma la zahanati iliyopo katika Kijiji cha Engusero Engine katika kata ya Chapakazi.

Machi 18, 2024, Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Vicent Gyunda  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, amefika katika eneo ambapo zahanati hiyo inajengwa na kuzungumza na viongozi wa chama na serikali, wajumbe wa kamati ya ujenzi na baadhi ya wananchi na kuwaeleza habari hiyo njema ya ukamilishaji wa zahanati hiyo.

Dr. Gyunda amesema kwamba pesa hiyo kwa kutamka ni nyingi ila kwenye utekelezaji ni ndogo  hivyo amewaomba wananchi kuendelea kutoa nguvu kazi.

“Nitoe rai kwenu, kila mtu anapaswa awe jicho kwenye pesa hizi. Pia viongozi mnapaswa kuwahabarisha wanakijiji wengine wajue nini kinaendelea”, aliongeza Dr. Gyunda.

Nae mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndg. Japhet Justani Kwanga, ameishukuru sana Halmashauri  ya Wilaya kwa kutenga pesa hizo na ameahidi  watatoa ushirikiano ili mradi upate kukamilika kwa wakati.

“Kwakweli  tunashukuru sana na tumefurahi kuona serikali ya Mheshiwa Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatujali” aliongeza Ndugu Kwanga.

Nae mmoja wa wananchi katika kijiji hicho, Ndg. Robert Abel Mpilimi ameshukuru ombi lao kusikilizwa na ameahidi kua wataunda kamati ya watu makini ili kuhakikisha mradi unakamilika vizuri na kwa wakati. “Sisi tumepewa fedha, kazi yetu sasa ni kutekeleza huu mradi ukamilike. Yaani wanasema Mungu akileta mvua haleti na wakulima ila sisi ndio wakulima hivyo serikali imeleta pesa kazi yetu  sisi kukamlisha mradi”, aliongeza Ndg. Mpilimi.

Nae Mtendaji wa Kijiji hicho ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo, Ndg Godwin Phabian Mbuya, amesema kwamba wanajiamini kwa nguvukazi, hivyo mradi utakamilika kwa wakati.

Wananchi wa kijiji hicho walianza na kukamilisha ujenzi wa boma hilo la zahanati mwaka 2020 baada ya kuwa wamekusanya michango ya ujenzi kwa muda wa miaka miwili. Mbali na nguvu kazi ya wananchi katika ujenzi wa boma hilo, pia limegharimu kiasi cha shilingi million 11.

Kukosekana kwa zahanati katika kijiji hicho kunawafanya wagonjwa na wajawazito wa kijijini hapo kwenda kupata huduma katika zahanati ya kijiji cha jirani, Osteti. Hali hii imekua adha kwao haswa katika kipindi cha masika ambapo daraja hufunikwa na maji na hivyo kuwafanya kushindwa kuvuka kwenda kupata matibabu. Umaliziwaji wa zanahati hiyo unatakiwa kukamilika ifikapo Juni 30,2024.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa