• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

SHULE ZA SEKONDARI KITETO ZATUNUKIWA VYETI KWA MAFANIKIO YA KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA PILI 2025

Imetumwa : February 12th, 2026

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Mhe. Athumani Kilimo, Februari 12, 2026, amekabidhi vyeti kwa shule za sekondari zilizofanya vizuri katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne na Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili mwaka 2025.

Akitoa taarifa ya matokeo hayo katika Kikao cha Baraza la Madiwani, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Mwl. Ally Kichuri, alisema kuwa kwa miaka mitatu mfululizo ufaulu umeendelea kuongezeka na kufikia asilimia 97.8 mwaka 2025. Alieleza kuwa mwaka 2026 wataalamu wataongeza juhudi ili kuhakikisha ufaulu huo unaendelea kupanda na kufikia asilimia 100, kama ilivyokuwa kwa watahiniwa wa Kidato cha Sita.

Katika hafla hiyo, Mhe. Kilimo alikabidhi vyeti vya pongezi kwa makundi mawili ya shule. Kundi la kwanza lilihusisha shule zilizokidhi vigezo vya KPI, ambapo shule sita zilitunukiwa vyeti kwa matokeo ya Kidato cha Nne, huku Shule ya Sekondari Kiteto ikikidhi kigezo hicho katika mtihani wa Kidato cha Pili.

Kundi la pili lilihusisha shule zilizofaulisha kwa asilimia 100, bila mwanafunzi yeyote kupata daraja sifuri. Shule tisa zilitunukiwa vyeti katika kundi hili, ikiwa ni ongezeko ikilinganishwa na matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2024, ambapo shule sita pekee zilifikia kiwango hicho.

Viongozi wa Chama na Serikali waliwapongeza wataalamu wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa usimamizi madhubuti wa sekta ya elimu, wakisisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za walimu, uongozi wa shule na ushirikiano wa jamii.

Utoaji wa vyeti mbele ya Baraza la Madiwani umeelezwa kuwa ni chachu ya kuongeza motisha kwa walimu na shule zote wilayani, huku ukiimarisha utamaduni wa ubora na ushindani chanya katika kuinua viwango vya ufaulu.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA MAPOKEZI YA FEDHA SEPTEMBA 2025 September 16, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU September 01, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHULE ZA SEKONDARI KITETO ZATUNUKIWA VYETI KWA MAFANIKIO YA KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA PILI 2025

    February 12, 2026
  • "FANYENI KAZI KWA KUZINGATIA NA KUIHESHIMU MIPAKA YA KISHERIA" – RC SENDIGA

    February 10, 2026
  • MAFUNZO MAALUMU KWA MADIWANI YAANZA WILAYANI KITETO

    February 09, 2026
  • JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI MAKAME KITETO YANYAKUA TUZO YA SERENGETI KWA UBORA WA UHIFADHI SHIRIKISHI

    February 02, 2026
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa