Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Ndg. Mufandii Msaghaa, ametoa rai kwa wananchi kudumisha amani na kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rai hiyo imetolewa AprilI 26,2025 katika kata ya Matui kwenye maadhimisho ya Muungano ngazi ya wilaya.
Mbali na kusisitiza kuutunza na kuuenzi Muungano, Ndg. Msaghaa alitoa pia rai ya kutunza amani haswa katika kipindi hiki ambapo nchi inaelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Aidha katika maadhimisho hayo, Katibu Tawala huyo alitoa zawadi kwa wananchi waliojibu vizuri maswali yahusuyo mambo ya Muungano.
Katika maadhimisho hayo, elimu mbalimbali ilitolewa ikiwa pamoja na elimu ya fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi ( mikopo ya 10%) na vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ambapo mjasiriamali akuwa nacho anaomba mkopo wenye riba ndogo na masharti nafuu kwenye benki NMB.
Aidha wananchi walipewa elimu jinsi ya kupambana na ukatili wa kijinsia pamoja na elimu kuhusu vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya siku 90.
Mbali na wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kutoa elimu mbalimbali, wananchi pia walipatiwa elimu kutoka kwa maafisa kutoka TAKUKURU, Mahakama na NIDA.
Maadhimisho hayo yalihitimishwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya timu kutoka Kibaya na timu ya Matui ambao Matui waliibuka kidedea kwa kuwafunga Kibaya magoli 3 kwa 0.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa