Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Ndg. Mufandii Msaghaa, wakati akiongoza kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Afua za Lishe cha Robo ya Pili ya mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika Januari 14, 2026.
Ndugu Msaghaa, aliwataka Watendaji wa Kata kuongeza juhudi katika maeneo ambayo hayajafanya vizuri kwenye Kadi Alama ili kufikia wastani mzuri wa utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe huku akiwahimiza kuendelea kuwahamasisha wazazi na walezi kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni kama njia ya kuimarisha lishe na mahudhurio ya wanafunzi.

Sambamba na hayo Ndugu Msaghaa aliwapongeza watendaji kwa jitihada zinazoendelea kufanyika katika kufikia viashiria vya mkataba wa lishe, akibainisha kuwa hali ya utekelezaji imeendelea kuimarika ikilinganishwa na awali.
Aidha, katika kikao kingine cha Kamati ya Lishe cha Wilaya kinachojumuisha wadau mbalimbali, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Ndg. Tellun Ndelwa, aliwataka Maafisa Kilimo kusimamia mashamba ya shule za msingi na sekondari ili kuwajengea wanafunzi uelewa wa kilimo kwa vitendo. Alieleza mpango huo utawasaidia wanafunzi kujifunza mbinu bora za kilimo, kutunza mazingira na kuelewa nafasi ya kilimo katika maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Lishe wa Wilaya, Ndg Catherine Massawe alieleza kuwa Wilaya ya Kiteto inaongoza katika Mkoa wa Manyara kwa kuwa na jumla ya mashine 11 za kuongeza virutubishi kwenye nafaka, hatua inayolenga kuongeza thamani ya mazao, kuboresha lishe kwa wananchi na kuimarisha usalama wa chakula.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa