• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAZAZI WASHIRIKISHWE MAVUNO YANAYOPATIKANA KWENYE MASHAMBA YA SHULE.

Imetumwa : January 16th, 2024

Watendaji wa Kata katika Halmashauri ya Wilaya Kiteto wameagizwa kuwashirikisha wazazi wa wanafunzi juu ya mavuno ya mazao yanayopatikana katika mashamba ya shule.

Hayo yamesemwa Januari 16, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh Remidius Mwema Emmanuel, katika kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe  ngazi ya kata na vijiji robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Idadi ya shule zinazotoa chakula shuleni na idadi ya wanafunzi wanaokula angalau mlo mmoja shuleni, ni mojawapo ya viashiria   vya utekelezaji wa mkataba huo wa lishe. Ili kuweza kutekeleza viashiria hivyo kwa 100%, ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kiteto ilitoa agizo kwamba katika msimu wa kilimo wa mwaka 2023/2024 kila shule wilayani hapo ilime angalu hekari tano za mahindi ili kuwapunguzia wazazi gharama ya  kuchangia chakula shuleni.

Mh. Mwema alisema kwamba inawezekana mavuno yasitosheleze chakula kwa wanafunzi kwa mwaka mzima hivyo ni busara baada ya mavuno watendaji kufanya hesabu ya kujua mavuno hayo yatatosheleza chakula kwa muda gani na kisha kutoa taarifa hiyo kwa wazazi ili wazazi wafahamu  kiasi gani kimepatikana na kiasi gani watapaswa kuchanga.

Aidha aliwapongeza watendaji ambao wamefamya vizuri katika kutekeleza mkatabata huo wa lishe kwenye kata zao. Kwa upande wa kata ambazo zilitekeleza chini ya lengo, Mh. Mwema amewaagiza watendaji wa kata hizo kuwashirikisha viongozi wa dini, mila na chama katika maeneo yao ili wawasaidie kuwahamasisha wananchi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji (W), CPA. Hawa Abdual Hassan, aliwasisitiza  watendaji hao kuendelea kusimamia vizuri suala la lishe shuleni kwani jambo hilo ni muhimu kwaajili ya wanafunzi na pia wilaya inapimwa kwenye utekelezaji wa mkataba huo wa lishe.

Kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya kata na vijiji kinafanyika kila robo ya mwaka kwa lengo la kujadili taarifa na viashiria vya lishe vilivyopo kwenye mkataba ambavyo vinatekelezwa kwenye ngazi ya kata na vijiji.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU September 01, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • DAS KITETO AWAHIMIZA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA UWEKEZAJI.

    September 11, 2025
  • UGONJWA WA HOMA YA INI (HEPATITIS B) NI TISHIO LA MAISHA LAKINI TUMAINI LIPO KUPITIA CHANJO

    September 04, 2025
  • DC MWEMA AFUNGUA RASMI ZAHANATI YA ENGUSERO SIDAN

    August 31, 2025
  • SAFARI YA KM 42 KUFUATA HUDUMA ZA AFYA SASA NI HISTORIA NDIRIGISHI

    August 30, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa