Mwenye koti katikati ni Hakimu Mkazi wa Kiteto Mh.Hudi Majid Hudi akiwa katika zoezi la kuwaapisha/kuwathibitisha wasimamizi wa Daftari la Wapiga kura Jimbo la Kiteto
Wasimamizi wa Daftari la Wapiga kura Jimbo la Kiteto wakiaapa/kuthibitisha tayari kwa uandikishaji.
Wasimamizi wa Daftari la Wapiga kura Jimbo la Kiteto wakisikiliza mada mbalimbali.
TAARIFA KAMILI .....
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kiteto Bw. Tamim H. Kambona ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, amefungua rasmi Mafunzo ya siku mbili (2)
ya Uboreshaji wa daftari la wapiga kura Jimbo la Kiteto kwa Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata leo tarehe 24.07.2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Zoezi hili la uandikishaji katika Jimbo la Kiteto litaanza tarehe 31.07.2019 hadi 06.08.2019 kwa kata zote 23 za Jimbo la uchaguzi Kiteto. Uandikishaji huu unatumia kifaa cha kisasa "Biometric Voters Registration kit (BVR KIT)" ambapo uchukuaji wa taarifa za mpiga kura zinachukuliwa kwa kutumia kompyuta, alama za vidole, saini ya kielektroniki na picha ambayo hairuhusu mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja kupitia mfumo wa usajiri wa wapiga kura "Voters Registration System.Malengo.
kazi na lengo kuu la kuboresha daftari la wapiga kura ni Kuandikisha wapiga kura wapya, kuboresha taarifa za wapiga kura hususani waliohama na wengineo, pia kuwaondoa wale ambao hawana sifa kama vile watu waliofariki.
Nani anaruhusiwa kuandikishwa?
Kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguz, Sura ya 343 na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ili mtu aweze kuwa mpiga kura anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:-
Awe raia wa tanzania - kwa kuzaliwa, kwa kurithi au kwa tajnisi (uraia wa kuomba),
Awe na umri wa miaka 18 au zaidi au atatimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya uchaguzi.
Agizo kwa wataalamu wanaohusika na Uboreshaji wa Daftari hili.
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kiteto Bw. Tamim H. Kambona amesema tuheshimu sana masuala yote yanayohusu uchaguzi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi. Kwa mtazamo huu nasisitiza wahusika wote wa zoezi la uandikishaji wapiga kura mfanye kazi kwa ushirikiano, bidii na weledi, pia kukaa katika kituo husika muda wote ili kufanikisha zoezi hili la uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Aliongeza kuwa wale ambao ni wazoefu basi wasifikiri wanajua kila kitu bali watumie fursa hii ya kuongeza ujuzi zaidi kisha wawe chachu ya utendaji kazi wenye matokeo chanya kwa Jimbo letu la Kiteto.
Uhamajishaji.
Kamati ya uhamasishaji zoezi hili litatoa matangazo kwenye mbao za matangazo kupitia tovuti ya Halmashauri ya Wialaya ya Kiteto, radio, runinga na kutumia magari ya yatayopita kitongoji kimoja hadi kingine ili kuwasisitiza wananchi wajitokeze kwa wingi katika uborehsji huu. Suala la uhamasishaji ni la msingi na litafanywa katika Jimbo lote la Kiteto na maeneo yote ya vijijini hadi ngazi ya Kitongojini kwa matangazo sahihi na kwa wakati kwani tunahitaji kuandikisha kwa asilimia mia moja (100%) katika Jimbo la Kiteto.
---------------------------------------------------- NAWASILISHA ------------------------------------------------------
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa