Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh. Remidius Mwema Emmanuel, amewaasa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kutengeneza misingi ya kutenda haki.
DC Mwema ameyasema hayo Februari 19, 2024 katika Mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika Kibaya, wenye lengo la kujitambulisha kwa wananchi na kusikiliza kero zao.
DC Mwema amesema kwamba, kiongozi anapaswa atende haki, hivyo ni lazma kiongozi atengeneze misingi ya kutenda haki.
Aidha DC Mwema amewaasa watumishi kuhusu masuala ya rushwa na kusema kwamba rushwa inanyima haki na pia mtumishi mmoja akipokea rushwa anafanya serikali ichukiwe na kuonekana kua serikali haitendi haki.
“Leo mtendaji mmoja wa kijiji akichukua rushwa, akawanyanyasa watu, anaifanya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, ionekane haitendi haki ni kwa uzembe wa mtu mmoja”, aliongeza DC Mwema.
Kuhusu migogoro ya ardhi wilayani hapo, DC Mwema amesema kwamba hafurahishwi na jinsi wilaya inavyosifika kwa migogoro.
DC Mwema amesema kwamba migogoro Kiteto itabaki historia na hivyo ameelekeza kila mmoja aliyepewa dhamana ya kuwajibika kama mtendaji na kiongozi kwenye nafasi yake ndani ya wilaya, atimize wajibu wake katika kuhakikisha migogoro iliyopo inatatuliwa na isizalishwe migogoro mipya.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa