Jengo la mama ngojea la hospitali ya wilaya ya Kiteto linavyoonekana kwa nje.
Jengo la mama ngojea la hospitali ya wilaya ya Kiteto linavyoonekana kwa ndani.
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto yajenga mama ngojea.
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto imejenga jengo la wakina mama wajawazito wanaosubiri kujifungua linalojulikana kama mama ngojea.
Mganga mfawizi wa hospitali ya wilaya ya Kiteto dakari Ramadhani Maingu amesema kwamba jengo la mama ngojea ni maalumu kwa ajili ya kina mama wanasubiri kujifungua ambao wanaviashiria vya hatari na wanaishi mbali na vituo vya afya au hospitali,kwamba badala ya kwenda kusubiria nyumbani ,watasubiri kujifungua wakiwa katika jengo hilo .
Aidha daktari Maingu amesema kwamba jego hilo lenye vyumba ya kulala ,sehemu ya kupumzikia ,chumba cha mhudumu wa afya , choo na bafu limeshakamilika na linakadiriwa kuwa na uwezo wa kuingia vitanda kumi na tano, na kwamba magodoro na vitanda viko tayari. Kilichobaki ni ujenzi wa vyoo vya nje, sehemu ya kufulia na jiko ambalo wakina mama hao watalitumia kujipikia wakati wakisubiri kujifungua.
Naye mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Bi Fatuma Kawia amesema kwamba jengo la mama ngojea ni muhimu sana. Katika vikao vya tathmini ya vifo vinavyotokana na uzazi ilionekana kwamba kuwa na jengo la mama ngojea katika vituo vya afya na hospitali ni moja wapo ya mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Kwa sababu wakati wa ujauzito mama akiwa anahudhuria kliniki na akagundulika kuwa na vidokezo vya hatari,ni bora akashauriwa azalie hospitali.Sasa kwa mama anayeishi mbali na kituo cha huduma akishafika mwishoni mwa ujauzito wake atapaswa kusogea na kujisubiria katika jengo la mama ngojea.
Katika hatua nyingine wakina mama waliohojiwa kuhusu jengo hilo la mama ngojea wamesema kwamba wanashukuru sana kwani litawaondolea adha ya kwenda kusubiria nyumbani ,kwani wakati mwingine wamekuwa wakija hospitali wakiwa na dalili za uchungu na wanalazimika kurudi nyumbani wasubiri hadi uchungu uchanganye,jambo ambalo linasababisha usumbufu kwani uchungu unapochanganya wakiwa majumbani kwao ambako ni mbali na vituo vya afya au hospitali na usafiri wa kuwafikisha hospitali wakati mwingine unachelewa kupatikana au kukosekana kabisa hasa nyakati za usiku ,hivyo kuhatarisha maisha yao na watoto walio tumboni.
Hadi sasa jengo hilo la mama ngojea limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni ishirini ,laki sita na elfu thelasini( 20,630,000), ambapo nusu ya fedha hizo zimetolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri .
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa