Kiongozi wa mbio za mwenge ndugu Amour Hamad Amour akisikiliza maelekezo ya jinsi mashine zinavyofanya kazi katika kiwanda cha Kwadelo Sunflower and Super kabla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo katika kata ya Matui.Aliyesimama kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Tumaini Magessa
Jengo la wodi ya wanawake na watoto lililozinduliwa na Mwenge wa uhuru katika kata ya Matui .
Jengo la madarasa yaliyozinduliwa na mwenge katika shule ya sekondari Engusero.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour akikagua darasa lililozinduliwa na mwenge katika shule ya sekondari Engusero katika kata ya Engusero.Walioambatana nae ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Tumaini Magessa,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kiteto Ndg. Tamim Kambona na maafisa wengine wa serikali wilayani Kiteto.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour akifungua mradi wa maji katika kata ya Kaloleni.
HABARI KAMILI
Wilaya ya Kiteto yatekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya kukuza uchumi wa viwanda.
Wilaya ya Kiteto imetekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka 2017 ambayo ni shiriki katika kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu, kwa kuanzisha kiwanda cha kukamua alizeti na kusaga mahindi.Kiwanda hicho kilichopo katika kata ya Matui ni miongoni mwa miradi minne iliyozinduliwa na mwenge wa uhuru wilayani kiteto.Mradi huo wa kiwanda una thamani ya shilingi 400,050,000.
Miradi mingine iliyozinduliwa na mwenge wa uhuru ni madarasa mawili yaliyojengwa katika shule ya sekondari Engusero iliyopo katika kata ya Engusero .Mradi huo wa madarasa una thamani ya shilingi 26,740,120,ambapo halmashauri imechangia shilingi 865,000 . Pia Kikundi cha vijana Kaloleni kilizinduliwa ,kikundi hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana kuendesha shughuli za kiuchumi na kukuza kipato cha kila kijana kwenye kikundi , kina miradi mbali mbali kama ufugaji kuku chotara, uuzaji wa vifaranga na mayai, kilimo cha mbogamboga, biashara ya bodaboda na VIKOBA, miradi yote hiyo ya kikundi cha vijana ina thamani ya shilingi 8,200,000 ,ambapo halmashauri ya wilaya ilikipatia kikundi hicho mkopo wa shilingi 2,000,000,fedha ambayo ilitumika kununua pikipiki, ambayo inawawezesha vijana hao kupata marejesho na kuendesha shughuli nyingine za kikundi. Mradi mwingine uliozinduliwa ni kampeni ya kutokomeza malaria, wilaya ya Kiteto ilianzisha kikundi cha kupambana na kutokomeza ugonjwa wa malaria.Mradi huo una thamani ya shilingi 500,000,ambapo fedha hizo zilitolewa na halmashauri .
Kadhalika mradi wa ujenzi wa jengo la wodi ya wanawake na watoto umewekewa jiwe la msingi.Mradi huo wa wodi upo katika kata ya matui na una thamani ya shilingi 37,796,000, halmashauri ya wilaya ya Kiteto imechangia shilingi 20,246,000 .
Sambamba na hayo, mradi wa maji ulifunguliwa . Mradi huo uko katika kata ya Kaloleni na una thamani ya shilingi 255,915,500, kati ya fedha hizo ,halmashauri imechangia shilingi 5,000,000.
Katika hatua nyingine miradi miwili ilikaguliwa. Miradi hiyo ni Kikundi cha wanawake, kikundi hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwawezesha wanawake kuendesha shughuli za kiuchumi na kukuza kipato na kina miradi kama kufuma mashuka ya kimasai ushanga ,kutengeneza shanga,hereni na mikufu ,usindikaji vyakula , uuzaji wa bidhaa mbalimbali kama sukari ,mchele na sabuni na VICOBA. Miradi yote hiyo ya kikundi cha wanawake ina thamani ya shilingi 10,500,000. Mradi mwingine uliokaguliwa ni mradi wa utunzaji wa mazingira, ambapo zoezi la upandaji miti katika eneo la shule ya Sekondari Engusero lenye ukubwa wa ekari 2.5 lilifanyika ikiwa ni sehemu ya utunzaji mazingira katika wilaya ya Kiteto. Mradi huo una thamani ya shilingi 1,420,000, ambapo halmashauri imechangia shilingi 160,000.
Mwenge wa uhuru umepokelewa wilayani Kiteto na mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa Tumaini Magesa, ambapo umepitia katika tarafa tatu,kata saba ,vijiji kumi na tano na kukimbizwa umbali wa kilometa 90 kutoka eneo la mapokezi hadi eneo la mkesha.Jumla ya miradi 8 imepitiwa na mwenge wa uhuru , thamani ya miradi yote iliyopitiwa ni shilingi za kitanzania 750,571,120, ambapo wadau wa maendeleo wamechangia shilingi 17,210,000 , Jamii shilingi 444,900,00, halmashauri ya wilaya ya Kiteto shilingi 28,771,000 na serikali kuu shilingi 259,690,120.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa