Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Charles Francis Kabeho akipokea taarifa ya ujenzi wa bweni la wavulana ( Mhe. John P.J Magufuli) lililojengwa katika shule ya sekondari ya Engusero.Mara baada ya kusomewa taarifa hiyo kabla ya ufunguzi wa bweni hilo.
Kiongozi wa mbio za mwenge Ndg. Charles Francis Kabeho akikagua vitanda vilivyopo ndani ya bweni la Mhe. John P.J Magufuli katika shule ya sekondari Engusero kabla ya kufungua bweni hilo, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru wilayani Kiteto.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho akikata utepe kama ishara ya kufungua bweni la Mhe. John P.J Magufuli katika shule ya sekondari Engusero wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Charles Francis Kabeho akipanda mti, kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa utunzaji mazingira. Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika katika shule ya sekondari Engusero wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho akijiridhisha kuhusu vipimo halisi vya barabara, kabla ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Namelock - Sunya .Tukio hili limefanyika Namelock wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho akizindua mradi wa maji katika mtaa wa Ngarenaro.Tukio hilo limefanyika wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwika ndoo ya maji mmoja kati ya wanawake wa mtaa wa Ngarenaro kama ishara ya ufunguzi wa mradi wa maji, uliojengwa katika mtaa huo. Tukio hilo limefanyika Ngarenaro wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.
................HABARI KAMILI...........
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu Charles Francis Kabeho ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa miradi ya maendeleo yenye viwango. Kabeho ametoa pongezi hizo wakati akifungua mradi wa bweni la wavulana katika shule ya sekondari Engusero lijulikanalo kama Mhe. John P.J. Magufuli .
Kabeho ametoa pongezi kwa Mkuu wa wilaya, Mwenyekiti wa halmashauri,Madiwani,Mkurugenzi mtendaji, wakuu wa idara ,pamoja na watumishi wote wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa usimamizi mzuri wa miradi pamoja na kujituma ambako kumesababisha kujengwa kwa bweni zuri, na kwa gharama ndogo.
Akisisitiza kuhusu pongezi hizo Kabeho amesema “ Kwanza niwapongeze Kiteto kwa jengo zuri, sambamba na kujenga bweni zuri, gharama ya shilingi 86,482,000 ni gharama ndogo,nikilinganisha na maeneo mengine ambapo tumekuta miradi ya ujenzi wa mabweni. Mabweni yamejengwa kwa gharama kubwa,lakini hayajafikia kiwango na uzuri huu,kuna wilaya ndani ya mkoa huu wa Manyara ambayo makadirio ya ujenzi wa bweni ni milioni 174,mpaka sasa wametumia milioni 89, lakini bweni halijafikia kiwango hiki.Natoa wito kwa halmashauri nyingine waje wajifunze Kiteto’’.
Wilayani Kiteto Mwenge wa Uhuru umepokelewa katika kijiji cha Ndaleta, baada ya mapokezi ,umekimbizwa umbali wa kilometa 108, ambapo umepita katika tarafa 4 ,kata 10 , vijiji 20, na na kukesha katika uwanja wa michezo wa Kibaya .Wakati wa mbio hizo jumla ya miradi 5 imepitiwa, kati ya hiyo , miradi 2 imefunguliwa ,miradi miwili imewekewa jiwe la msingi, na mradi mmoja wa utunzaji mazingira,ambapo katika mradi wa utunzaji mazingira, zoezi la upandaji miti limefanyika katika shule ya sekondari Engusero.
Aidha thamani ya miradi yote ni shilingi za Kitanzania 6,996,805,804, ambapo wahisani wamechangia Sh. 6,411,919,000 /= ,jamii sh. 400,000,000,halmashauri ya wilaya Sh. 30,192,000/= na serikali kuu Sh.154,694,804/=.
Ujumbe wa mwenge wa uhuru mwaka 2018 ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha,wekeza sasa kwa maendeleo ya nchi yetu’.
.............MWISHO............
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa