Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander .Mnyeti Akizungumza Katika Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Kilichofanyika Katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mjini Kibaya Tarehe 28.05.2020.
Kutoka Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi.Beatrice Rumbeli, wapili ni Mh.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel na watatu ni Mh.Mwenyekiti wa CCM Wilaya Omari Kiondo.
Mh.Mbunge wa Wilaya ya Kiteto Emmanuel Papian Akisalimia Wajumbe wa Baraza Hilo.
Hao hapo juu ni Waheshimiwa Madiwani Wakiwa katika Kikao Hicho
Mh.Diwani Viti Maalumu Chadema Zamzam Said Akizungumza Wakati Anatoka Chadema Kuhamia CCM Siku Hiyo Hiyo ya Kikao cha Baraza la Madiwani Mbele ya MH. Mkuu wa Mkoa wa Manyara A. Mnyeti.
Mh.Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kiteto Omari Kiondo (aliyevaa shati la kijani) akikabidhiwa Kadi ya Chadema na Mh.Diwani Viti Maalumu Chadema Zamzam Said (kulia mwenye kitambaa cheupe) Ambaye amehamia Rasmi Kuingia CCM, wa Katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Kiteto Bi.Neema Nyalege
Waheshimia Madiwani na Wajumbe Mbalimbali Walisimama Kama Ishara ya Kumpongeza na Kumpokea Mh. Diwani (Viti Maalum) Zamzam
-------------------------------------- HABARI KAMILI -----------------------------------------
Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo katika uongozi wake kwa miaka ya fedha ya 2016/17,2017/18 na 2018/19 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali.
Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mnyeti alitoa pongezi hizo akiwa katika ziara ya kuhudhuria Baraza la Madiwani kwa kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali yaliyofanyika katika makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mjini Kibaya tarehe 28.05.2020.
“Kwa kweli lazima niwapongeze Waheshimiwa Madiwani, Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel, Mh.Mkuu wa Wilaya Mhandisi T. Magessa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona, Wakuu wa Idara na Vitengo na Wataalam wote wa Halmashauri kwa kuhakikisha mnapata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo kwani miaka ya nyuma hali haikuwa kama ilivyo sasa, hongereni sana” Alisema Mh.Mkuu wa Mkoa huyo.
Pamoja na pongezi hizo pia alimtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali kuhakikisha baadhi ya hoja kama za upungufu wa watumishi na kupewa ukuu wa Idara/Kitengo zinaondolewa kwa Halmashauri kwa kuwa hizo ni hoja za kisera na kamwe hazihusiani na Madiwani kwani Madiwani hawana uwezo wa kutatua tatizo la upungufu katika Halmashauri.
Aidha Mh. Mkuu aliendelea kwa kusisitiza, “Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali kuna baadhi ya hoja kwa kweli ni vema mkawakague Wizara ya Utumishi na TAMISEMI ndo muwaulize kwanini hawaleti watumishi na kuwapandisha vyeo watumishi waliokaimu Idara/Vitengo kwa muda mrefu Mkoa wa Manyara” Akijibu hoja hiyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Mkoa wa Manyara Bwana Paschal Mawago alisema kuwa watajitahidi kukaa na wataalam wa Halmashauri kuhakikisha kuwa hoja zote za kisera zinafutwa na pia aliwataka wataalam kufika katika Ofisi za Mkaguzi zilizopo Babati wakati wowote wapatapo vielelezo vya baadhi ya hoja ili kuzifuta na kuzifunga.
Hata hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuwa juu zaidi kwa kuvuna wanachama mbalimbali toka vyama vya upinzani kwani katika Baraza hili la Madiwani Wilayani Kiteto Mh.Mkuu wa Mkoa alishuhudia Diwani wa viti Maalum Mh. Zamzam Said kutoka CHADEMA alitumia nafasi hiyo kukihama chama chake na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Mheshimiwa Mwenyekiti kuanzia leo tarehe 28.05.2020 mimi nikiwa kama Diwani wa CHADEMA nimeamua kujiunga na CCM bila kushawishiwa na mtu yoyote kwani sioni jambo la maana watakalofanya CHADEMA ambalo Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli hajafanya. Alisema Mheshimiwa Zamzam.
Mh.Mkuu wa Mkoa pia alitumia ziara hiyo kuwaaga na kuwatakia kila la heri Madiwani na Wabunge wote wa Mkoa wa Manyara kwani Mabaraza yote ya Madiwani yanayotarajiwa kuvunjwa kuanzia tarehe 10 .06.2020 ili kupisha mchakato wa uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais kuanza. pia aliwataka Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia ipasavyo rasilimali za Halmashauri katika kipindi hicho ambacho Halmashauri hazitakuwa na Mabaraza ya Madiwani.
“Kwa kuwa hili ni Baraza la mwisho kabla ya Baraza kuvunjwa nitumie nafasi hii kuwatakia kila la heri Madiwani katika uchaguzi ujao wa mwezi Oktoba, naamini zaidi ya 90% mtarudi baada ya uchaguzi, lakini katika kipindi hiki nawataka Mh. Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia ipasavyorasilimali zote ili kuhakikisha mnadhibibiti matumizi ya fedha” Alisisitiza Mh. Mkuu wa Mkoa huyo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa