Kuanzia kushoto ni Bw. Partrick Mlay ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa nje, Bw. Stefano Ndaki - Katibu Tawala Wilaya ya Kiteto, Bw. Tamim Kambona
Afisa Mwandikishaji Mkuu ngazi ya Jimbo na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Eng. Tumaini Magessa.
HABARI KWA UFUPI.....
Katika ukaguzi huo Mkuu wa Wilaya Mh. Eng.Tumaini Magessa amesisitiza Afisa Mwandikishaji Ngazi ya Jimbo Bw. Tamim Kambona ahakikishe uhamasishaji unakuwa wa kutosha kwa kila eneo lakini pia na wahusika wote wanaoendesha zoezi hili wawe mabalozi wazuri kuanzia sasa hadi kuisha kwa zoezi hili kwa Jimbo letu la Kiteto ili wananchi wajitokeze kwa wingi kwani ndiyo mafanikio Serikali inayoyataka.
Mkuu wa Wilaya Mh. Eng. Magessa amewaasa wahusiaka kuzingatia mafunzo haya elekezi kwa faida ya nchi yetu, kwani Serikali imetumia rasilimali nyingi kuwekeza katika rasilimali watu na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika zoezi hili ili kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa apate haki yake.
Mh. Eng. Magessa aliongozana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Bw. Stefano Ndaki pamoja na Afisa Mwandikishaji Ngazi ya Jimbo Bw. Tamim Kambona.
------------------------------------------------------------------- NAWASILISHA -----------------------------------------------------------------
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa