Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akitoa pongezi na maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona na kaimu Mhandisi wa ujenzi wilaya Mhandisi Chogo Mang'era baada ya kukagua ujenzi wa uzio wa hospitali ya wilaya ya Kiteto wakati alipotembelea hospitalini hapo.
Uzio wa Hospitali ya wilaya ya Kiteto ambao ujenzi wake unaendelea ni moja wapo ya miradi ya maendeleo ambayo inasimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa ufanisi mkubwa.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti pamoja na ujumbe wake wakiwasili katika jengo la idara ya wagonjwa wa nje (OPD) wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto.Aliyesimama upande wake wa kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti pamoja na ujumbe wake wakiingia katika wodi ya wanaume wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akiwa ndani ya wodi ya wanawake akipokea maelezo kuhusu upatikanaji wa vifaa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto Dkt. Malkiadi Mbota wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akiwa ndani ya jengo la upasuaji akipokea maelezo kuhusu uhaba wa wataalamu wanaoshughulika na upasuaji kutoka kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Kiteto Dkt. Malkiadi Mbota wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto.
Watumishi katika jengo la upasuaji hospitali ya wilaya ya Kiteto wakiwa tayari kuendelea na majukumu yao ya kila siku.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akiwa ndani ya jengo la kitengo cha dawa na vifaa tiba hospitali ya wilaya ya Kiteto akitoa maelekezo kuhusu udhibiti wa dawa wakati alipotembelea hospitalini hapo.
....... HABARI KAMILI........
RC MNYETI AMPONGEZA DED KITETO
Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo .Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa uzio wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto alipotembelea hospitalini hapo mapema wiki hii.
Akizungumza wakati wa kukagua uzio huo mheshimiwa Mnyeti anasema ‘‘mkurugenzi kazi yako ni nzuri ,ukuta huu kujengwa kwa shilingi milioni 32 ni matokeo ya usimamizi mzuri. Nashauri miradi yote mtakayoendelea kuitekeleza itumie force account ili thamani ya fedha ionekane, nimependa sana kazi hii, kazi nzuri sana, pesa iliyotumika kidogo’’.
Akiwa hospitalini hapo mheshimiwa Mnyeti pia amemtaka mganga mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DMO) daktari Malkiadi Paschal Mbota kuhakikisha kwamba hakuna dawa inayo potea. Akisisitiza kuhusu udhibiti wa dawa mheshimiwa Mnyeti anasema ‘‘Mheshimiwa mkuu wa wilaya hakikisha dawa zinadhibitiwa . DMO sisi tuna wataalamu wetu wanatupa taarifa , tukibaini kwamba umeshindwa kusimamia madaktari wako , dawa zinapotea ovyo ovyo tutakuondoa''.
Aidha mheshimiwa Mnyeti amemuagiza daktari Mbota kuhakikisha kwamba dawa zinapotolewa hospitali ya wilaya kwenda katika vituo vya afya, kamati za dawa katika vituo vya afya zipokee dawa,na zinapopokea zidhibiti matumizi ya dawa katika vituo hivyo ili dawa ziwafikie wananchi. Pia amemuagiza DMO kutoa semina za mara kwa mara juu ya umuhimu wa kudhibiti dawa kwa kamati za dawa na watumishi wanaohusika na utoaji dawa .Vilevile mheshimiwa Mnyeti amewataka watumishi wa kitengo cha dawa na vifaa tiba kudhibiti upotevu wa dawa ili kuongeza tija katika utumishi wao.
Katika ziara hiyo mheshimiwa Mnyeti alitembembelea maeneo mbalimbali ya hospitali ikiwemo kitengo cha madawa na vifaa tiba, jengo la upasuaji , wodi ya wanaume ,wodi ya wanawake pamoja na jengo la idara ya wagonjwa wa nje (OPD), ambapo amewapongeza madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kwa kazi wanayofanya kuokoa maisha ya watu, na kuwatia moyo kwamba kazi wanayofanya ni kazi ya wito , waendelee kuongeza bidii kuwatumikia wananchi katika wito huo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa