Maandamano ya Wafanyakazi wakiongozwa na Jeshi la Polisi na Bendi ya Matarumbeta toka Makao Makuu ya Wilaya kwenda Uwanja wa Mpira
Wafanyakazi wakipita katika Jukwaa Kuu kwa Mgeni Rasmi
Wafanyakazi katika Ishara ya Mshikamano daima
Katibu wa CWT - Kiteto (W) Mwl.Rosemary Mwakibete akisalimia Wafanyakazi
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe hii Bi. Zahra Goda akisoma Risala kwa usaidizi wa Bw. Msechu
Vikundi vya Taasisi mbalimbali katika uimbaji wa Mashairi
Sherehe hii ilijaa Burudani na Michezo mbalimbali ya kufukuza kuku na kuvuta kamba kwa vyama vyote
Mtumishi kutoka Idara ya MIPANGO - Bw. Edgar P. Kavenuke akipokea Cheti cha Mfanyakazi Hodari na fedha taslimu.
Baadhi ya Wafanyakazi Hodari wakipokea Vyeti na Fedha Taslimu zilizoanzia Tshs. 200,000/= hadi 500,000/=
Baadhi ya Wafanyakazi Wastaafu kwa mwaka huu wa fedha wakipokea zawadi za Bati toka vyama vyao
Mwenyekiti wa Halmashauri (W) Kiteto Mh. Lairumbe Mollel akipokea Cheti cha Utambuzi
Mkurugenzi Mtendaji (W) akivishwa taji baada ya kupokea Cheti cha Pongezi kwa kujipambanua zaidi juu ya Kusimamia maendeleo ya Wilaya yake kwa dhati mpaka kuweka kambi Kata ya Kijungu na Sunya, Kutenda Haki na Uwazi.
Wanakikundi akina Mama wa CWT Kiteto katika Ujasiliamali wa kutengeneza nguo mbalimbali, Batiki "Boutique", Mashela kwa wanandoa, Shanga, Heleni, Bangili nk, wapo Community Centre Kibaya Mjini.
Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw. Tumaini Magessa akikagua bidhaa na kupata taarifa fupi toka kwa Mwenyekiti wa Kikundi husika. Mgeni Rasmi aliongozana na Viongozi wa Chama Tawala (CCM) na Taasisi mbalimbali za Wilayani Kiteto katika ukaguzi huu kama wanavyoonekana hapo juu.
Kimsingi tasnia ya Viwanda ni pana kwa hiyo kuongeza thamani ya vitu, kuzalisha na mbinu wezeshi za kimasoko zitasaidia kuongeza kipato na kutoa ajira kwa anayethubutu na kujituma katika kazi hivyo aliwapongeza sana washiriki wa Kikundi hiki.
Mgeni Rasmi ambaye ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw. Tumaini Magessa akizungumza jambo na wachezaji baada ya kukagua timu hizo.
Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw. Tumaini Magessa akizungumza jambo katika Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika usiku kwenye Ukumbi wa Community Centre Mjini Kibaya. Mgeni Rasmi alisisitiza, Wafanyakazi wote kufanya kazi kwa uaminifu na kuonyesha tija.
Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Tamim Kambona akishukuru jambo ambapo ilifahamika kwamba leo ni siku yake ya kuzaliwa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa