Mhandisi Thadeo Mwangonela wa Shirika la OIKOS EAST AFRICA Akiwasilisha Mada Kwa Wadau wa Maji.
Bw. Tamilwai William wa Shirika la OIKOS EAST AFRICA Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kiteto Mhandisi Stephano Mbaruku Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Kwa katikati ni Afisa Mipango wa Wilaya ya Kiteto Bi. Beatrice Rumbeli Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Kulia ni Kaimu Afisa Usafi na Mazingira Wilaya ya Kiteto Bw. Keveratus Sibanganya Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji, Kushoto ni Afisa Mipango Wilaya ya Kiteto Bi. Beatrice Rumbeli.
Bw. Beatus Temba Akimuwakilisha (Afisa Elimu Msingi Wilaya) Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Aliyesimama ni Mchumi Bw. Edgar Kavenuke Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Aliyesimama ni Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Rodrick Kidenya Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Aliyesimama ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Joseph Zablon Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Dr. P. Mbota Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Aliyesimama ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Irkiushbour Bw. Haiyo Loltikise Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Aliyesimama ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Makame Bw. Shaban Katanga Akitoa Ufafanuzi Katika Uwasilishaji wa Mada Kwa Wadau wa Maji.
Hao Hapo Juu ni Picha Mbalimbali za Kikao Hicho.
------------------------------------------ HABARI KAMILI ----------------------------------------------
Hayo yamethibitishwa leo tarehe 11.11.2019 katika kikao cha wadau wa maji kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri wa Wilaya ya Kiteto. Akizungumza katika mafunzo ya uimarishaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira Wilayani Kiteto, Mhandisi Thadeo Mwangonela wa Shirika la OIKOS EAST AFRICA amesema kuna shilingi za kitanzania bilioni 5 zitakazowekezwa kwenye miradi ya maji katika Wilaya mbili Simanjiro na Kiteto kwa muda wa miaka 3 kuanzia mwaka huu wa fedha 2019/2020. Mradi huu utajikita katika sekta nne za kipaumbele yaani Afya, Elimu, biashara na Maji ambapo katika afya, elimu na biashara ni ujenzi wa vyoo vya kisasa vyenye kutumia maji, wakati huo huo katika jamii ambazo hazina maji basi watawekeza katika hilo ili kuondoa adha ya maji kulingana na mahitaji ya eneo husika. Kwa sasa kabla ya mradi kuanza kunatakiwa kufanyika kwa vikao na mafunzo katika ngazi mbalimbali kuanzia Wilaya hadi Vijijini ili kutoa taarifa hizi na kufanya utafiti wa kimahitaji (need assessment) kwa kila Wilaya.
Meneja wa Wakala wa maji mjini na vijijini (RUWASA) Mhandisi Stephano Mbaruku amesema hadi sasa Wilaya ya Kiteto kwa takwimu za maji Vijijini inajumla ya 38.3% ya upatikanaji wa maji vijijini lakini kwa uwekezaji huu wa sasa tutakuwa na uwezo wa kufikia 80% kwa kipindi cha miaka 3 ijayo kama kutakuwa na ushirikiano mzuri baina ya wananchi, RUWASA na OIKOS.
Kwa mara nyingine tena Meneja wa RUWASA Mhandisi Stephano Mbaruku amekemea sana suala la viongozi wa maeneo husika hususani Maafisa Watendaji wa Vijiji na Maafisa Watendaji wa Kata kutofumbia macho suala la uharibifu wa miundombinu ya miradi ya maji katika maeneo yao, ili kuonekana kwa thamani ya fedha za miradi hiyo kwa wananchi.
Katika kuhakikisha miradi hii inakuwa salama na endelevu viongozi katika ngazi za Kata, Vijiji na Vitongoji watumie mbinu suluhishi zitakazopunguza au kuondoa kabisa dhana potofu ya kuharibu miradi kwa kutumia sheria ndogo ndogo, kukaa na wazee mashuhuri wa maeneo husika na kuweka ulinzi shirikishi wa kijamii ili kulinda miundombinu ya maji katika mradi husika.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto iko tayari kushirikiana na RUWASA ili kuleta maendeleo endelevu ya maji kwa wananchi wa Kiteto, hata hivyo wameshukuru Shirika la OIKOS kwa kuisaidia Serikali na jamii ya Kiteto kwa ujumla wake kwenye sekta tajwa hapo juu, chamsingi waendelee kuwa nasi bega kwa bega ili kuhakikisha maendeleo ya uhakika yanapatikana na sisi kama serikali tuko tayari kutumia fedha hizi kwa malengo yaliyokusudiwa tu na si vinginevyo.
Katika kuwepo wa miradi hii wadau wamesema la msingi ni kwamba kabla ya kuanza mradi ni muhimu zoezi husika la upembuzi yakinifu likawa la kutumia muda mfupi wa siku zisizozidi 30 na wataalamu wa Shirika hili la OIKOS wamekubali kuwa itakuwa hivyo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa