Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim H. Kambona.
............HABARI KAMILI................
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona amesema kwamba Halmashauri yake itaweka nguvu katika miradi yote ya ujenzi wa miundo mbinu ya elimu ili kuunga mkono juhudi za wananchi sambamba na kuwezesha majengo hayo kuweza kutumika ili kupunguza changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa,mabweni na nyumba za walimu wilayani hapa.Kambona ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya uongozi ya Halmashauri cha kujadili na kupitisha bajeti kilichofanyika Jumatatu ya tarehe 28-01-2019 kwenye ukumbi wa halmashauri .
Akizungumza wakati wa kikao hicho Kambona amesema “ Tunawajibu wa kukamilisha miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,mabweni pamoja na nyumba za walimu ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi.Majengo hayo yanavyoendelea kukaa tu kama maboma bila kumaliziwa, tunawavuja moyo wananchi.Wametumia nguvu na mali zao, ni lazima na sisi tuonyeshe kwamba tunajali juhudi zao,tutakuwa tukikamilisha jengo moja baada ya jingine kwa kadiri tutakavyokuwa tukipata fedha .”
Kambona amekuwa akifanya jitihada kubwa sana katika kuhakikisha kwamba Halmashauri yake inapiga mbio katika suala zima la maendeleo.Hadi sasa ,chini ya uongozi wake, miradi mbalimbali ya maendeleo yenye viwango vya ubora vya hali ya juu imetekelezwa.Mfano kwenye sekta ya elimu; madarasa ,vyoo na mabweni yamejengwa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari, mengine yamekarabatiwa,sambamba na unuzi wa samani kama meza,viti,vitanda na magodoro ili kuwawezesha watoto wanaosoma katika shule mbalimbali wilayani hapa,kusoma katika mazingira mazuri.
...........MWISHO.......
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa