Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kiteto Ndg. Robert Urassa.
Hatua Mbalimbali za Uvamizi kama inavyoonekana katika picha.
...........HABARI KAMILI.............
Afisa Kilimo wa wilaya ya Kiteto Ndugu Robert Urassa amewataka wakulima na wafugaji wilayani Kiteto kuchukua tahadhari dhidi ya aina mpya ya viwavi waitwayo Viwavi Vamizi . Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia kuwepo kwa viwavi Vamizi ( Fall Armyworm au FAW) -Spodoptera frugiperda (J.E. Smith). Ndugu Urassa ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya idara yake kuhusu viwavi hao wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Halmashauri ( CMT) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto .
Akitoa taarifa hiyo ndugu Urassa amesema kwamba sababu ya kuwepo kwa viwavi hao ni hali ya hewa katika msimu wa kilimo 2017/2018 ambayo imechangia uwepo wa mazingira mazuri ya ustawi wa wadudu wengi katika mzunguko wa maisha yao ulioandamana na mwenendo wa ustawi wa mimea hasa mazao, hali iliyosababisha kujitokeza kwa matukio kadhaa ya Mbilizi au Viwavi – jeshi (African Armyworm) na hata Viwavi Vamizi (Fall Armyworm) wilayani Kiteto.
Katika taarifa yake ndugu Urassa amesema kwamba hadi kufikia Mwezi Februari, 2018 Viwavi hao wameathiri eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 370.4 za zao la mahindi na Hekta 12 za malisho katika kata za Partimbo ,Makame,Bwagamoyo,Kaloleni,Kibaya,Lengatei,Magungu, Sunya na Matui. Ameelezea kiwango cha athari katika mimea iliyoshambiliwa ambapo amesema kwamba kiwango hicho ni wastani wa 20% ,ambacho kimesababishwa hasa na wadudu walioshambulia wakiwa mmoja mmoja au katika makundi madogo madogo .Ndugu Urassa amefafanua kwamba hapakuwa na tukio la athari lililosababishwa na viwavi wakiwa katika kundi kubwa kiasi cha kuleta mlipuko (‘‘Armyworm” Outbreak).
Aidha ndugu Urassa amesema kwamba mwendelezo wa mashambulizi ya viwavi hao yameweza kuongezeka kwa kasi sana kutokana na hali ya hewa iliyokuwepo wilayani kote katika kipindi cha mwezi Januari hadi Februari 2018. Hata hivyo wataalamu wa kilimo wa halmashauri wanafanya jitihada za dhati katika kutoa ushauri na maelekezo kwa wakulima kuhusu jinsi ya kutumia viuatilifu sahihi na kwa wakati ili kudhibiti viwavi hao . Amesisitiza kwamba jambo kubwa , na la msingi kwa wakulima ni kufanya ukaguzi wa mazao yao shambani mara kwa mara ili kufanya udhibiti mapema mara dalili zitakapoonekana .Sambamba na hayo, ndugu Urassa ametoa angalizo kwamba kuna viashiria vya kutokea kwa athari ya kiwango kikubwa zaidi katika kipindi kifupi na kirefu kijacho,katika maeneo mengi wilayani Kiteto ikiwa viwavi hao hawatadhibitiwa ipasavyo.
Kadhalika ndugu Urassa ameainisha changamoto zilizopo katika kukabiliana na viwavi hao , changamoto hizo ni ; ugeni wa viwavi vamizi na mtindo wake wa kushambulia mimea kufanana na ule unaofanywa na viwavi jeshi waliozoeleka kiasi cha kutobainika mapema pale wanapofanya mashambulizi wakiwa katika makundi madogo madogo sana, uwezo mdogo wa wakulima wengi kumudu gharama za kununua viuatilifu na wigo mpana wa mimea mbadala walionao viwavi vamizi kiasi cha kuhitaji udhibiti wake uhusishe pia maeneo ambayo si mashamba.
Katika hatua nyingine ndugu Urassa ameainisha hatua mbalimbali zilizochukuliwa na idara yake katika kukabiliana na mlipuko wa Viwavi Vamizi. Hatua hizo ni ; Kutoa taarifa za tahadhari kwa Umma kupitia serikali za vijiji kwa kuziandikia barua yenye kumbukumbu namba HMW/KT/K/119/VOL.11/26 ya tarehe 30/01/2018.Kutoa maelekezo ya kitaalamu kwa wataalamu wote wa ugani kuhusu namna ya kuvitambua Viwavi Vamizi ,pamoja na hatua za kufanya ili kukabiliana na matukio ya wadudu hao pindi watakapojitokeza, kupitia barua yenye kumbukumbu namba KI/KIT/T/14/152 ya tarehe 15/01/2018.Kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu hatua za udhibiti zinazostahili kuchukuliwa.Kufanya mawasiliano na kitengo cha afya ya mimea, ofisi ya kanda ya kaskazini – Arusha kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kupatiwa viuatilifu vya kukabiliana na tatizo hilo . Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani inatarajia kununua viuatilifu kidogo kiasi cha lia 100 ili kusaidia jitihada za wakulima katika udhibiti wa Viwavi Vamizi.
Vilevile Urassa amesema kwamba baada ya kufanya mawasiliano na Kitengo cha afya ya mimea - kanda ya kaskazini (Arusha ) ,majibu waliyoyapata ni kwamba kitengo hicho hakina viuatilifu hivyo. Hata hivyo ndugu Urassa amesema kwamba wizara ya kilimo imekwisha idhinisha aina za viuatilifu ambavyo vinaweza kutumika katika kudhibiti. Viuatilifu hivyo ni pamoja na;Duduba 450 EC ,Dudual ,Belt 480 SC,Mupcron 50 EC,Protrin 60 EC .Pia ndugu Urassa amesema kuwa pamoja na kwamba halmashauri iko kwenye mchakato wa kununua lita 100 za viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti viwavi hao, kiasi hicho ni kidogo sana kulinganisha na mahitaji yaliyopo,hivyo wakulima wanunue viuatilifu kwa gharama zao .
Viwavi Vamizi (Fall Armyworm) ni aina mpya ya Viwavi jeshi ambayo asili yake ni katika bara la Amerika, viwavi hao wameanza kujitokeza katika nchi za Afrika ( Tanzania ikiwemo) kuanzia msimu wa kilimo 2016/2017.Viwavi hao ambao ni viluilui au viwavi wa Nondo ,wana sifa ambazo zinawafanya kuwa tishio kubwa.Wana uwezo wa kushambulia mimea zaidi ya aina 80 ikiwemo mazao, malisho na hata magugu pamoja na uwezo wa nondo kusafiri angani kwa zaidi ya kilometa 500. Pia wanauwezo wa kushambulia mmea ukiwa katika hatua zote za ukuaji hadi ukomaaji, na kuendelea kusababisha uharibifu kwa kipindi kirefu,ambapo wanaweza kukamilisha mzunguko wa maisha yao katika kipindi cha siku 28- 30 na kurudia mashambulizi upya.
Mzunguko-maisha wa Viwavi-vamizi:
Mzunguko-maisha (The life cycle) wa Viwavi-vamizi hukamilishwa kwa muda unaotofautiana kutegemeana na kiwango cha joto, pamoja na hali nyingine za mazingira zilizopo katika eneo husika, kwa vile huathiriwa sana na baridi kali. Yaani, Mzunguko-maisha huu, hukamilishwa katika kipindi cha kama siku 30 katika kipindi cha Kiangazi, siku 60 katika Masika, na siku 80 hadi 90 katika kipindi cha Kipupwe. Hali hii husababisha Wadudu hawa kuzaa vizazi 6 – 12 kwa Msimu mmoja, japo katika kipindi chote cha maisha, Kiwavi-vamizi jike anauwezo wa kutaga hadi mayai 1,500 – 2,000.
Mbinu za udhibiti:
Viwavi-vamizi hudhibitiwa kwa kutumia mbinu mbalimbali kuanzia zile za kiasilia hadi zile za kutumia Kemikali-kilimo. Mbinu hizo ni kama ifuatavyo:
ØMatumizi ya Kanuni Bora za Kilimo katika kuendesha shughuli za kilimo, kama vile kupanda kwa wakati, kupalilia kwa wakati, n.k.
ØMatumizi ya mbegu-kinzani (Tolerant/Resistant Varieties)
ØMatumizi ya viumbe rafiki katika kuwadhibiti Viwavi-vamizi hao, kama vile Telenomus romus, Trichogramma Spp., Diapetimorpha introit.
ØMatumizi ya baadhi ya Bakteria wenye uwezo wa kuvishambulia na kuviangamiza kama vile Baccilus thuringiensis, meterihzium anisoplie, n.k.
Ø Matumizi ya viuatilifu sahihi kwa wakati wake
-Nyunyiza Viuatilifu, asubuhi au jioni, huu ukiwa ni wakati ambapo Viwavi-vamizi hushambulia zaidi.
-Weka mchanganyiko sahihi, wa maji na Viuatilifu kama ilivyoshauriwa na kuelekezwa kwenye kibandiko.
-Dhibiti Viwavi-vamizi vikiwa bado vidogo katika hatua zake za awali kabla havijajificha.
Wilayani Kiteto Watakiwa Kuchukua Tahadhari Dhidi ya Viwavi Vamizi.
Afisa Kilimo wa wilaya ya Kiteto Ndugu Robert Urassa amewataka wakulima na wafugaji wilayani Kiteto kuchukua tahadhari dhidi ya aina mpya ya viwavi waitwayo Viwavi Vamizi . Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia kuwepo kwa viwavi Vamizi ( Fall Armyworm au FAW) -Spodoptera frugiperda (J.E. Smith). Ndugu Urassa ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya idara yake kuhusu viwavi hao wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Halmashauri ( CMT) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto .
Akitoa taarifa hiyo ndugu Urassa amesema kwamba sababu ya kuwepo kwa viwavi hao ni hali ya hewa katika msimu wa kilimo 2017/2018 ambayo imechangia uwepo wa mazingira mazuri ya ustawi wa wadudu wengi katika mzunguko wa maisha yao ulioandamana na mwenendo wa ustawi wa mimea hasa mazao, hali iliyosababisha kujitokeza kwa matukio kadhaa ya Mbilizi au Viwavi – jeshi (African Armyworm) na hata Viwavi Vamizi (Fall Armyworm) wilayani Kiteto.
Katika taarifa yake ndugu Urassa amesema kwamba hadi kufikia Mwezi Februari, 2018 Viwavi hao wameathiri eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 370.4 za zao la mahindi na Hekta 12 za malisho katika kata za Partimbo ,Makame,Bwagamoyo,Kaloleni,Kibaya,Lengatei,Magungu, Sunya na Matui. Ameelezea kiwango cha athari katika mimea iliyoshambiliwa ambapo amesema kwamba kiwango hicho ni wastani wa 20% ,ambacho kimesababishwa hasa na wadudu walioshambulia wakiwa mmoja mmoja au katika makundi madogo madogo .Ndugu Urassa amefafanua kwamba hapakuwa na tukio la athari lililosababishwa na viwavi wakiwa katika kundi kubwa kiasi cha kuleta mlipuko (‘‘Armyworm” Outbreak).
Aidha ndugu Urassa amesema kwamba mwendelezo wa mashambulizi ya viwavi hao yameweza kuongezeka kwa kasi sana kutokana na hali ya hewa iliyokuwepo wilayani kote katika kipindi cha mwezi Januari hadi Februari 2018. Hata hivyo wataalamu wa kilimo wa halmashauri wanafanya jitihada za dhati katika kutoa ushauri na maelekezo kwa wakulima kuhusu jinsi ya kutumia viuatilifu sahihi na kwa wakati ili kudhibiti viwavi hao . Sambamba na hayo, ndugu Urassa ametoa angalizo kwamba kuna viashiria vya kutokea kwa athari ya kiwango kikubwa zaidi katika kipindi kifupi na kirefu kijacho,katika maeneo mengi wilayani Kiteto ikiwa viwavi hao hawatadhibitiwa ipasavyo.
Kadhalika ndugu Urassa ameainisha changamoto zilizopo katika kukabiliana na viwavi hao , changamoto hizo ni ; ugeni wa viwavi vamizi na mtindo wake wa kushambulia mimea kufanana na ule unaofanywa na viwavi jeshi waliozoeleka kiasi cha kutobainika mapema pale wanapofanya mashambulizi wakiwa katika makundi madogo madogo sana, uwezo mdogo wa wakulima wengi kumudu gharama za kununua viuatilifu na wigo mpana wa mimea mbadala walionao viwavi vamizi kiasi cha kuhitaji udhibiti wake uhusishe pia maeneo ambayo si mashamba.
Katika hatua nyingine ndugu Urassa ameainisha hatua mbalimbali zilizochukuliwa na idara yake katika kukabiliana na mlipuko wa Viwavi Vamizi. Hatua hizo ni ; Kutoa taarifa za tahadhari kwa Umma kupitia serikali za vijiji kwa kuziandikia barua yenye kumbukumbu namba HMW/KT/K/119/VOL.11/26 ya tarehe 30/01/2018.Kutoa maelekezo ya kitaalamu kwa wataalamu wote wa ugani kuhusu namna ya kuvitambua Viwavi Vamizi ,pamoja na hatua za kufanya ili kukabiliana na matukio ya wadudu hao pindi watakapojitokeza, kupitia barua yenye kumbukumbu namba KI/KIT/T/14/152 ya tarehe 15/01/2018.Kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu hatua za udhibiti zinazostahili kuchukuliwa.Kufanya mawasiliano na kitengo cha afya ya mimea, ofisi ya kanda ya kaskazini – Arusha kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kupatiwa viuatilifu vya kukabiliana na tatizo hilo . Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani inatarajia kununua viuatilifu kidogo kiasi cha lia 100 ili kusaidia jitihada za wakulima katika udhibiti wa Viwavi Vamizi.
Vilevile Urassa amesema kwamba baada ya kufanya mawasiliano na Kitengo cha afya ya mimea - kanda ya kaskazini (Arusha ) ,majibu waliyoyapata ni kwamba kitengo hicho hakina viuatilifu hivyo. Hata hivyo ndugu Urassa amesema kwamba wizara ya kilimo imekwisha idhinisha aina za viuatilifu ambavyo vinaweza kutumika katika kudhibiti. Viuatilifu hivyo ni pamoja na;Duduba 450 EC ,Dudual ,Belt 480 SC,Mupcron 50 EC,Protrin 60 EC .Pia ndugu Urassa amesema kuwa pamoja na kwamba halmashauri iko kwenye mchakato wa kununua lita 100 za viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti viwavi hao, kiasi hicho ni kidogo sana kulinganisha na mahitaji yaliyopo,hivyo wakulima wanunue viuatilifu kwa gharama zao .
Viwavi Vamizi (Fall Armyworm) ni aina mpya ya Viwavi jeshi ambayo asili yake ni katika bara la Amerika, viwavi hao wameanza kujitokeza katika nchi za Afrika ( Tanzania ikiwemo) kuanzia msimu wa kilimo 2016/2017.Viwavi hao ambao ni viluilui au viwavi wa Nondo ,wana sifa ambazo zinawafanya kuwa tishio kubwa.Wana uwezo wa kushambulia mimea zaidi ya aina 80 ikiwemo mazao, malisho na hata magugu pamoja na uwezo wa nondo kusafiri angani kwa zaidi ya kilometa 500. Pia wanauwezo wa kushambulia mmea ukiwa katika hatua zote za ukuaji hadi ukomaaji, na kuendelea kusababisha uharibifu kwa kipindi kirefu,ambapo wanaweza kukamilisha mzunguko wa maisha yao katika kipindi cha siku 28- 30 na kurudia mashambulizi upya.
Mzunguko-maisha wa Viwavi-vamizi:
Mzunguko-maisha (The life cycle) wa Viwavi-vamizi hukamilishwa kwa muda unaotofautiana kutegemeana na kiwango cha joto, pamoja na hali nyingine za mazingira zilizopo katika eneo husika, kwa vile huathiriwa sana na baridi kali. Yaani, Mzunguko-maisha huu, hukamilishwa katika kipindi cha kama siku 30 katika kipindi cha Kiangazi, siku 60 katika Masika, na siku 80 hadi 90 katika kipindi cha Kipupwe. Hali hii husababisha Wadudu hawa kuzaa vizazi 6 – 12 kwa Msimu mmoja, japo katika kipindi chote cha maisha, Kiwavi-vamizi jike anauwezo wa kutaga hadi mayai 1,500 – 2,000.
Mbinu za udhibiti:
Viwavi-vamizi hudhibitiwa kwa kutumia mbinu mbalimbali kuanzia zile za kiasili hadi zile za kutumia Kemikali-kilimo. Mbinu hizo ni kama ifuatavyo:
Matumizi ya Kanuni Bora za Kilimo katika kuendesha shughuli za kilimo, kama vile kupanda kwa wakati, kupalilia kwa wakati, n.k.
Matumizi ya mbegu-kinzani (Tolerant/Resistant Varieties)
Matumizi ya viumbe rafiki katika kuwadhibiti Viwavi-vamizi hao, kama vile Telenomus romus, Trichogramma Spp., Diapetimorpha introit.
Matumizi ya baadhi ya Bakteria wenye uwezo wa kuvishambulia na kuviangamiza kama vile Baccilus thuringiensis, meterihzium anisoplie, n.k.
Matumizi ya viuatilifu sahihi kwa wakati wake
Nyunyiza Viuatilifu, asubuhi au jioni, huu ukiwa ni wakati ambapo Viwavi-vamizi hushambulia zaidi.
Weka mchanganyiko sahihi, wa maji na Viuatilifu kama ilivyoshauriwa na kuelekezwa kwenye kibandiko.
Dhibiti Viwavi-vamizi vikiwa bado vidogo katika hatua zake za awali kabla havijajificha.
............. MWISHO .............
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa