Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Kiteto CPA. Hawa Abdul Hassan, amezindua mradi wa vyoo matundu manne na mabafu manne katika Shule ya Msingi Partimbo iliyopo Kata ya Partimbo baada ya vyoo vya awali kutitia mwezi Desemba 2023.
Uzinduzi huo umefanyika shuleni hapo Februari 12, 2024 na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Mh. Kassimu Msonde Diwani wa Kata ya Kibaya, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Partimbo Ndugu Kimerei Masiaya pamoja na wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, wazazi, walimu wa shule ya Msingi Partimbo na shule jirani pamoja na wanafunzi.
Akisoma taarifa ya mradi huo kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji (W), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Mariamu Abdallah Swalehe, amesema kwamba ujenzi huo ambao umegharimu jumla ya kiasi cha fedha 17,857,000 ulianza kutekelezwa Desemba 15, 2023 na umekalimika Februari 9, 2024.
Aidha Mwalimu Mkuu huyo amesema kwamba kukamilika kwa mradi huo kumeondoa adha ya wanafunzi wasichana 164 ambao walikua wanalazimika kutembea mita zaidi ya 100 kufata vyoo vya SWASH wakati wa usiku.
Vilevile Bi. Mariamu alishukuru kwa ushirikiano walioupata kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuanzia kipindi cha maandalizi, utekelezaji na hatimaye ukamilikaji wa mradi huo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji (W), amesema kwamba ameufurahia mradi huo ambao umetekelezwa katika ubora na aliupongeza uongozi wa shule, mwenyekiti wa Kamati ya Shule, jamii na walimu kwa kuusimamia vizuri na hatimaye kukamilika kwa wakati.
Pia aliwaasa wanafunzi wanufaika wa mradi huo kuthamini mradi huo kwa kutunza usafi wa vyoo hivyo na mabafu hayo.
Pia alitoa ombi kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, kamati ya shule na jamii kuanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana wenye uhitaji maalumu ambao utagharimu kiasi cha fedha 128,000,000 kutoka serikali kuu.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, Ndugu Papakinyi Kaai, ameupongeza uongozi wa shule, kamati, jamii pamoja na Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya Ndugu Felician Mbugi kwa usimamizi wao mzuri wa mradi huo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa