Kushoto ni Maafisa Usajili wa NIDA na kulia ni Wateja wao ambao kwa hatua ya awali Mteja huingia katika chumba hiki ili kupokea taarifa kwa utaratibu maalum kama wanavyoonekana hapo juu.
Zoezi lililopo kwa sasa ni la usajili kwa Wananchi kwa Kata za jirani yaani Kibaya na Kaloleni tu, kisha Kata zingine zitafuata. Kila muhusika lazima aanzie katika Ofisi za Serikali za Mitaa kisha utaelekezwa kuja Ofisi ya NIDA Wilaya ambazo zipo katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto jengo la Idara ya Maji (W) karibu kabisa na Ofisi za TANESCO Wilaya ya Kiteto.
Zoezi la uchukuaji wa Vitambulisho vya Uraia katika Ofisi ya NIDA Wilaya ya Kiteto kwa Watumishi wote umesitishwa hadi hapo Ofisi ya Usajili Nida (W) itakapotoa taarifa.
Kushoto ni Afisa Usajili wa NIDA Bi. Beatrice Muhina akimuelekeza mwananchi taratibu za kufanya kapitia vifaa husika ili kuwezesha kuingiza taarifa za Mteja huyu kwenye Mfumo wa kujisajili.
Afisa Usajili wa NIDA Bi.Beatrice Muhina (kushoto) akiingiza taarifa za Mteja kwa hatua mbalimbali.
Kimsingi, kwa sasa wananchi wote wa Kata ya Kibaya na Bwagamoyo wanakaribishwa kujisajili, ni muhimu na vitambulisho hivi ni bure kwa kila mwananchi.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Afisa Usajili (W) Bi.Beatrice Muhina Ofisi ya NIDA Wilaya ya Kiteto.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa