Mh.Mkuu wa Wilaya Mhandisi Tumaini Magessa Akifungua Kikao Hicho Kilichofanyika Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
Aliyesimama ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona Akiwasalimia Wajumbe wa Kikao Hicho.
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona, Wapili ni Mh.Mkuu wa Wilaya Mhandisi Tumaini Magessa, wa Tatu ni Afisa Kilimo Mkuu Bi. Margaret Natai wa Wizara ya Kilimo Toka Dodoma kwa Kushirikiana na Mwisho ni Afisa Kilimo Mkoa wa Manyara Bw.Samweli Dahaye WAkiwa na Wadau wa Kikao Hicho.
Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wadau wa Usalama wa Chakula Wilayani kiteto Mh. Diwani wa Kata ya Kaloleni, Christopher Parmet Ambaye Aliteuliwa na Wajumbe siku Hiyo Hiyo ya Kikao.
Afisa Kilimo Mkuu Bi. Margaret Natai wa Wizara ya Kilimo Toka Dodoma Akiwasilisha Mada.
Afisa Kilimo Mkoa wa Manyara Bw.Samweli Dahaye Akiwasilisha Mada.
-------------------------------------------------------------------------------- HABARI KAMILI -------------------------------------------------------------------------------------
Hayo yamejulikana katika kikao cha tarehe 06.03.2020 katika mafunzo ya wadau wa usalama wa chakula wilayani kiteto yaliyofunguliwa na Mh.Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Katika ufunguzi huu Mh. Mkuu wa Wilaya Mhandisi Tumaini Magessa alisisitiza kwamba tuwe na jukwaa lenye matokeo chanya kwa wananchi kwani ndiyo lengo kuu la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt J.P.Magufuli. Aliendelea kusema ili tufanikiwe katika usalama wa chakula ni lazima tuwe na data sahihi zitakazowezesha kuwa na ufahamu wa nini kinaendelea ili kufanya maamuzi sahihi. Hata hivyo kila mtu ajiulize atakumbukwa kwa lipi alilolifanya hapa kiteto na duaniani kwa ujumla wake kwa wenzake na taifa.
Afisa Kilimo Mkuu Bi. Margaret Natai wa Wizara ya Kilimo toka Dodoma kwa kushirikiana na Afisa Kilimo Mkoa wa Manyara Bw.Samweli Dahaye ndiyo walioendesha mafunzo ya wadau wa wilaya, kuhusiana na usalama wa chakula. Ili kufanikisha hili kuna nyanja tatu za kufanyia kazi mwanzo ni mkakati wa kusimamia mazao, mpango wa kutekeleza huo kakati na mwisho ni muongozo wa namna ya kupanga haya majukwaa.
Yote haya yanafanyika ikiwa ni malengo mahususi ya kusambaza na kutoa elimu kwa wadau, kuandaa kanzi data ya wadau yuko wapi na anafanya nini kwani taarifa hizi ni za muhimu sana katika kufanya maamuzi. Kimsingi imefahamika kwamba baada ya mavuno kuna upotevu wa uwingi wa mazao, ubora na hatimae inapelekea kushuka kwa thamani ya mazao husika hivyo kuathiri mfumo wa uchumi wa nchi. Katika mazao haijabagua ni mazao ya makundi yote yanayolimwa na kuvunwa baadhi ni mazao ya nafaka kama vile mahindi,maharagwe, mpunga na ngano, mazao ya mafuta kama vile alizeti na karanga, mazao ya mizizi kama vile mihogo na viazi aina zote.
Dira katika usalama wa chakula ni kuhakikisha tunapunguza kiwango cha upotevu wa mazao na dhima ni kuboresha usimamizi wa mazao baada ya kuvuna. Kuna vitu vya msingi kadhaa vya kufahamu katika usalama wa chakula hususani sababu zinazopelekea kuendelea kupungua kwa mazao baada ya mavuno hapa nchini; baada ya kufanyiwa uchambuzi wa kina kitaalamu imejulika kuwa ni uelewa mdogo wa wananchi wote wanaojihusisha na shuguli za mnyororo wa mazao kuanzia yanapokuwa shambani hadi kumfikia mlaji, teknolojia duni, miundombinu ya masoko isiyona na tija kwa wadau, kutokuwepo kwa barabara zinazopitika kwa urahisi katika baadhi ya sehemu na kutokuwa na mfumo wa kupata taarifa sahihi za masoko nchni. Kutofanyika kwa utafiti wa namna jambo lilivyo, usimamizi duni wa kanuni na miongozo, Uwezo mdogo wa taasisi mbalimbali katika kushugulikia hili, masuala mtambuka kama vile athari za mabadiliko ya tabia nchi, uwekezaji mdogo wa kifedha na mwisho ni ukosefu wa takwimu sahihi na taarifa zote hizi hupelekea mazao mbalimbali kupungua baada ya mavuno.
Hata hivyo wadau wote walieleza kwamba kwa uelewa wao suala kubwa ni kutokuwepo kwa masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi hii kupelekea thamani ya zao husika kuwa ndogo ukilinganisha na gharama za mkulima anazoingia kuanzia kulima, kupalilia, madawa ya shambani na baada ya kuvunwa, gharama za kuvuna, usafirishaji kwenda kutafuta masoko na kuhifadhi gharani au nyumbani, miundombinu ya usafirishaji na kuwepo kwa umeme wa uhakika ili mwananchi aweze kutumia zana mbalimbali ili aweze kuongeza thamani ya zao husika baada ya mavuno.
Mwisho liliundwa jukwaa la wadau wa usalama wa chakula wilayani kiteto ambapo Mwenyekiti aliteuliwa Mh. Diwani wa Kata ya Kaloleni, Christopher Parmet. Jukwaa hili liliundwa kwa kuzingatia makundi mbalimbali kama vile wauzaji wa pembejeo, taasisi za kifedha, wasafirishaji wa mazao, wanunuzi, wabunifu wa teknolojia, watafiti, wanasiasa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs na CBOs).
Kazi ya jukwaa hili ni kufanya ushawishi wa kila siku kwa wananchi maeneo mbalimbali katika wilaya yetu, kudumisha utekelezaji wa jukwaa, kuielewa na kutekeleza dhima, kufanya tathmini kwa kuangalia yale yaliyoazimiwa na kikao je yanatekelewa pia mdau yeyote wa jukwaa hili ili aweze kutoka ni lazima aandike barua ya kujitoa yeye mwenyewe.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa