Siku moja baada ya mafunzo kwa Makarani waongozaji wapiga kura kukamilika, Tume Huru ya Taifa Uchaguzi Jimbo la Kiteto, imeendelea na mafunzo kwa Wasimamizi wa Vituo na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo mafunzo ambayo yameanza leo Oktoba 27, 2025 na yanatarajiwa kukamilika Oktoba 27,2025.
Akizungumza katika mafunzo hayo katika Kituo cha Maktaba, Mgeni Rasmi wa Kituo hicho Ndg. Godfrey Mwangairo amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwazi na uaminifu mkubwa katika kipindi chote cha uchaguzi.

Mafunzo hayo ambayo yanayoendelea katika vituo vinne vyenye jumla ya washiriki 1, 726, yamelenga kuwajengea uwezo wasimamizi hao ili waweze kuongoza vituo vya kupigia kura kwa ufanisi na kwa kuzingatia taratibu zote zilizowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Ndg. Mwangairo alisema wasimamizi wa vituo ni nguzo muhimu katika kuhakikisha zoezi la upigaji kura linafanyika kwa amani, uwazi na uhalali wa kidemokrasia.
“Ninyi ndiyo viongozi wakuu wa vituo vya kupigia kura hivyo, uadilifu wenu ndio utakaolinda imani ya wananchi na vyama vya siasa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Fanyeni kazi kwa haki, bila upendeleo wala uonevu,” alisisitiza Ndg. Mwangairo.
Aidha, aliwakumbusha wasimamizi hao kuzingatia kanuni za uchaguzi, taratibu za upigaji na kuhesabu kura, pamoja na umuhimu wa kushirikiana na mawakala wa vyama vya siasa bila ubaguzi.
Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wamepongeza juhudi za INEC katika kuwaandaa watendaji wa uchaguzi kwa ufanisi, wakisema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa na kuondoa sintofahamu kuhusu majukumu yao siku ya uchaguzi.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa