Kusimamia na kufuatilia ukusanyaji wa taka katika vizimba,uzoaji taka kutoka vizimbani kwenda dampo kuu.Kazi hii inafanywa na jamii kwa kushirikiana na mzabuni ambaye huzoa taka tripu 30 za lori kutoka katika vizimba viwili.
Kusimamia utekelezaji wa sheria namba 1 ya mwaka 2003 ya mamlaka ya chakula, dawa na vipodozi (TFDA).
Ufuatiliaji wa ubora wa majengo yote yanayotumika katika biashara za vyakula ikiwemo kuhifadhi ,kuuza na kuzalisha vyakula baada ya kukidhi vigezo.Majengo hayo yameanza kupatiwa usajili .
Kuratibu shughuli za usafi siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kama ilivyo agizo la Rais ,pamoja na siku ya usafi ya Alhamisi ya kila wiki kama lilivyo agizo la halmashauriUsimamizi na utekelezaji katika ngazi ya wilaya ,kata na vijiji umekuwa ukifanyika,timu ya wilaya ikiongozwa na mkuu wa wilaya inafanya jukumu la kusimamia utekelezaji kiwilaya.kata ikiongozwa na afisa mtendaji wa kata inasimamia kata,na kupokea taarifa zote kwa watendaji wa vijiji.Watendaji wa vijiji wanashirikiana na jamii kusimamia usafi na kutuma taarifa kwa mtendaji wa kata.
Kubuni mbinu za kupendezesha mji mdogo wa kibaya,ambapo idara hufanya mikutano na wadau wa usafi katika mji wa kibaya. Katika mikutano wa tarehe 13/04/2018 maazimio yafuatayo yaliwekwa.
Kutekeleza sheria za upendezeshaji mji mara moja na kuwachukulia hatua wote wanaochafua mji kwa kutupa taka hovyo.
Kufuatilia uwepo wa mapipa ya taka katika maeneo ya biashara,hususani maeneo ya maduka na migahawa.
Kuwaandikia barua wakuu wote wa taasisi ,kuwataka kufyeka nyasi ,kuondoa vichaka katika maeneo yao na kupanda miti ya kisasa ya kivuli na maua yenye kulenta mandhari nzuri ya mji.