Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan, anawakumbusha wananchi wote kua kliniki ya Madaktari Bingwa inaendelea katika Hospitali ya Wilaya iliyopo Kibaya.
Madaktari Bingwa ambao wanaendelea na huduma katika Hospitali ya Wilaya ni pamoja na Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Ukunga, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto na Bingwa wa Magonjwa ya Kinywa na Meno. Wengine ni pamoja na Bingwa wa Magonjwa ya Ndani, Bingwa wa Upasuaji na Bingwa wa Dawa za Usingizi na Ganzi.
Gharama za Uchangiaji zinazotumika kupata huduma hizi za kibingwa ni zile za siku zote zinazotozwa na Hospitali ya wilaya. Aidha bima za afya bima wanahudumiwa kupitia bima zao.
Wananchi wote mnahimizwa kujitokeza ili kuweza kupata huduma hii adhimu.
Kumbuka: AFYA NI MTAJI.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa