Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. CPA. Hawa Abdul Hassan Desemba 8, 2025 katika mafunzo yaliyoandaliwa na Halmashauri kwa vikundi vilivyokidhi vigezo vya kupata mkopo wa Halmashauri wa 10% katika Robo ya kwanza ya mwaka 2025/26.
CPA Hawa alisisitiza umuhimu wa kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa, hususan kutekeleza miradi waliyoiomba, akibainisha kuwa serikali imeweka rasilimali hizo kwa dhamira ya kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Wilaya ya Kiteto.
“Nawasisitiza mikopo hiyo mtakayopewa iende ikatumike kama fursa kwenu ya kujikomboa kiuchumi kutoka hatua moja kwenda nyingine lakini kumbukeni kurejesha kwa wakati ili iwe endelevu na wengine waweze kunufaika”, alisema CPA. Hawa.
Aidha, aliwapongeza vikundi vilivyopita vilivyoonesha nidhamu ya marejesho, akisema hatua yao imekuwa chachu ya mafanikio ya mpango huo, huku akiwataka wachache wanaochelewesha kurejesha kubadilika ili wasirudishe nyuma juhudi za serikali katika kuwawezesha wananchi.
Mwisho, CPA Hawa aliwahakikishia wanavikundi kuwa fedha walizoomba zitaingizwa kwenye akaunti zao kufikia Desemba 12 , hivyo aliwataka kujiandaa kuanza utekelezaji wa miradi yao mara moja.
Mafunzo hayo yametolewa kwa wanavikundi kutoka kata za Kibaya, Partimbo, Kaloleni na Bwagamoyo, ambapo walipatiwa elimu na miongozo mbalimbali ya kuwaimarisha katika usimamizi wa mikopo na utekelezaji wa miradi yao.
Ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za serikali za kuwawezesha wananchi kupitia mikopo isiyorudishwa na riba, katika robo ya kwanza ya mwaka 2025/26, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 248 kwa vikundi 97 ambavyo zimekidhi vigezo vyote vinavyohitajika katika kupata mkopo wa 10% unaotolewa na Halmashauri.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa