Maendeleo ya ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi katika Kata ya Kaloleni wilayani Kiteto. Mradi huu pamoja na mengine inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto inadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya msingi ya elimu bora na mazingira rafiki ya kujifunzia.
Mradi huu unajumuisha ujenzi wa madarasa sita ya elimu ya msingi pamoja na vyoo matundu kumi kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya msingi. Aidha, mradi huu inajumuisha vyumba viwili vya madarasa ya awali, vyoo matundu sita kwa wanafunzi wa awali pamoja na uzio katika shule ya awali hatua inayoonesha uwekezaji wa kimkakati katika kuimarisha misingi ya elimu kuanzia ngazi ya awali.

Mbali na hayo mradi huu unajumuisha jengo la utawala pamoja na vyoo vya walimu matundu mawili.

Mradi upo katika hatua ya umaliziaji na kukamilika kwa mradi huu wenye thamani ya shilingi 330,700,000, kutapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Kaloleni yenye jumla ya wanafunzi 1,594, sambamba na kupunguza umbali mrefu ambao wanafunzi wanatembea kufuata elimu. Mradi huu ni ushahidi wa vitendo wa ahadi ya serikali ya kusogeza huduma za elimu karibu na wananchi na kujenga kizazi kizazi chenye maarifa kwa maendeleo ya Taifa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa