Maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, mradi wenye thamani ya shilingi milioni 800 unaotekelezwa kwa ufadhili wa Serikali Kuu. Ujenzi wa Mradi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto umefika 28 %.Kukamilika kwa jengo hili kutaimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi kwa kupunguza msongamano wa wagonjwa, kuongeza ufanisi wa huduma za matibabu, kuboresha mazingira ya kazi kwa wahudumu wa afya na kusogeza huduma bora, salama na za kisasa zaidi karibu na wananchi wa Wilaya ya Kiteto na maeneo ya jirani.Halmashauri ya Wilaya ya kiteto inatoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya uimarishaji wa huduma za afya na kuendelea kujali maslahi ya wananchi wa Wilaya ya Kiteto.

Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa