• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

ATAKAYEKWAMISHA ZOEZI LA CHANJO YA SURUA RUBELLA KUCHUKULIWA HATUA

Imetumwa : February 16th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh Remedius Mwema Emmanuel, amesema kwamba yupo tayari kumchukulia hatua mtu yoyote atakayekwamisha zoezi la chanjo ya Surua Rubella inayoendelea nchi nzima.

Mh Mwema ameyasema hayo Februari 16, 2024 kwenye Ukumbi wa Maktaba katika kikao cha PHC (Primary Health Care) kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Surua Rubella Wilaya ya Kiteto.

Mheshimiwa Mwema amesema kwamba suala la chanjo ni ajenda ya Kitaifa  na anahitaji wilaya yake iwe ya kwanza katika Mkoa, hivyo hatopenda kuona mtu yoyote akikwamisha zoezi hilo na hivyo kwa yoyote ambaye atakwamisha zoezi la chanjo wilayani hapo atamchukulia hatua. “Wilaya kua ya kwanza inawezekana maana kua wa kwanza kunahitaji kuratibu na kushirikiana” aliongeza Mh. Mwema.

Lengo la kikao hicho ilikua ni kutoa elimu juu ya Kampeni ya Chanjo ya Surua Rubella inayoendela nchini kwa watoto wenye umri wa miezi 9 hadi miezi 59.

Mh Mwema amesema kwamba kupeana elimu kunasaidia kupata uelewa na viongozi wakielewa wataenda kuelimisha jamii na hivyo kuondoa dhana potofu.

                                                                                                           

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Huduma za Afya, Bi Elizabeth Joseoh Urio, amesema kwamba wananchi wanapaswa waelezwe umuhimu wa chanjo hiyo.” Wapo watu ambao wanaacha kuwapeleka watoto chanjo haswa wakiona kuna watu wengi hivyo wanaona wanapoteza muda wao ila wakifahamu umuhimu wa chanjo watahakikisha watoto wao wanapata chanjo” aliongeza Bi. Elizabeth.

Nae Mganga Mkuu wa Wilaya, Dr. Vicent Gyunda, amesema kwamba wamejipanga kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa kuhakikisha wanafikia lengo na pia wanavuka lengo la uchanjaji.

                                                                                                       

Halmashauri ya Wilaya Kiteto inalenga kuchanja watoto 57,435. Mpaka kufikia siku ya pili ya Kampeni hiyo Februari 16,2024, Halmashauri imeweza kuchanja jumla ya watoto 34,418 ambapo ni sawa na 59.93% ya lengo la uchanjaji.

Chanjo ya Surua Rubella inatolewa bure kwa watoto walio na umri kuanzia miezi 9 hadi miezi 59 katika Hospitali ya Wilaya, Vituo vya Afya vyote, Zahanati zote na katika vituo maalumu  vilivyoteluliwa kwa muda kutoa huduma hiyo. Kampeni hii ina lengo la kuongeza kinga kwa walengwa.

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa