Katika tukio la kipekee lililowagusa wakimbiza Mwenge Kitaifa na umati wa wananchi wa Ngabolo, mama mmoja amejifungua mtoto wa kiume masaa machache kabla ya uzinduzi wa jengo jipya la zahanati ya Ngabolo uliokuwa ukifanywa na Mwenge wa Uhuru.
Akitoa taarifa hiyo kwa furaha kwa Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, alisema kwamba mama huyo amefurahia sana kujifungua siku hiyo ambayo ni muhimu na maalumu katika zahanati hiyo na kwa kuonesha furaha hiyo ameamua kumpa mwanae jina 'Ismail' ambalo ni jina la Mkimbiza Mwenge wa Kitaifa.
Mkimbiza Mwenge kitaifa, Ndg. Ismail Ali Ussi, alipopewa taarifa hiyo, aliguswa na tukio hilo na kuonesha furaha yake kwa heshima hiyo kubwa aliyopewa.
"Ni jambo la kipakee sana, nimefurahi sana kusikia habari hii. Na kuonesha furaha hii mimi pamoja na wakimbiza Mwenge wenzangu tunatoa zawadi ya shilingi laki tano kwa mtoto huyu", alisema Ndg. Ussi.
Zahanati hiyo ni miongoni mwa miradi mbalimbali inayozinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa