Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za maendeleo zilizopokelewa wilayani hapa katika kipindi cha miaka mitano ambayo wamekaa madarani.
Pongezi hizo zimetolewa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Robo ya Tatu 2024/2025 kilichofanyika Aprili 29-30, 2025 wilaya hapa. Madiwani hao wamesema kwamba fedha nyingi zimeletwa katika halmashauri na hakuna kata imekosa fedha kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto amesema kwamba Rais Samia alipata uongozi katika kipindi kigumu ambacho dunia ilikua inapitia kwani kilikua kipindi ambacho kuna janga la ugonjwa wa korona na kutokana na hilo uchumi wa dunia ulikua umedorora ila aliweza kulivusha taifa katika kipindi hicho kigumu.
“Kwa ushupavu wake ameliongoza taifa vizuri katika kipindi hicho kigumu. Lakini pia tunampongeza kwa usimamizi mzuri wa miradi yote ya kimkatati katika taifa iliyokua imeachwa na Hayati Dr. John Pombe Magfuli, ikiwemo Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na mradi wa treni ya mwendo kasi”, ameongeza Mhe. Bundala.
Aidha baraza hilo mbali na kumpongeza Mhe. Rais Samia, limetoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji, CPA. Hawa Abdul Hassan pamoja na timu ya wataalam kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato na usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa.
“Bajeti ya Halmashauri imeongezeka kutoka 2.5bilioni mwaka 2020/2021 hadi kufikia 4.9 kwa mwaka ujao wa fedha 2025/2026. Kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kumeiwezesha halmashauri kupeleka fedha nyingi kwenye miradi ili kuhakikisha miradi inakamilika”, ameongeza Mh. Bundala.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa