Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Abdallah Bundala, Februari 6,2025 limepitisha rasimu ya Mpango wa Bajeti ya kiasi cha zaidi ya TZS 38.9 bilioni kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Akiwasilisha rasimu hiyo ya bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, Ndg. Tellun Ndelwa, amesema katika Mwaka wa Fedha 2025/26, halmashauri inapanga kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka TZS 3.9 bilioni hadi TZS 4.5. Kiwango hicho ni sawa na ongezeko la 15.1% ukilinganisha na mpango wa bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa