Halmashauri ya Wilaya Kiteto imepokea takribani kiasi cha fedha shilingi bilioni 13.7 kwaajili kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya, Elimu, Utawala, Kilimo na Mifugo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan Novemba 22, 2023 Babati Mjini kwenye mkutano na waandishi wa habari wa kueleza miradi ya maendeleo inayotekezwa katika Mkoa wa Manyara.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi huyo amesema kwamba katika kipindi cha serikali ya Awamu ya Sita ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kiteto imetekeleza miradi yenye thamani ya takribani bilioni 6.4 kwenye sekta ya elimu ilhali miradi iliyotekelezwa katika sekta ya afya imegharimu takribani bilioni 2.7.
Upande wa sekta ya Kilimo na mifugo, Kiteto imetekeleza miradi yenye thamani ya kiasi cha fedha takribani bilioni 2.6 na idara ya Utawala wilaya imetekeleza miradi yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 2.
“Tunazidi kuishukuru serikali ya awamu ya sita ya Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusikia na kuzifikia changamoto za wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Tunamuombea siha njema yeye pamoja na wasaidizi wake ili waendelee kuwahudumia watanzania” alisema ndugu Hawa Abdul Hassan.
Mkutano huo ambao ulirushwa mubashara na kituo cha runinga cha ITV, ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndugu Mobhare Matinyi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mh Queen Sendiga. Pia mkutano huo ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakiwemo wakuu wa Wilaya zote ndani ya Mkoa wa Manyara na Wakurugenzi watendaji wote katika Mkoa wa Manyara, watumishi pamoja wananchi wa mkoani Manyara.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa