Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan, akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi.
Ofisi ya Mkurugenzi imeandaa kitabu hicho cha maombolezo kwaajili ya watu kusaini katika kipindi hiki cha maombolezo.
Mkurugenzi anawakaribisha viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, taasisi za serikali na binafsi, watumishi wa umma pamoja na wananchi wote kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kusaini kwenye kitabu hicho cha maombolezo.
Kitabu cha Maombolezo pia kinapatikana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kiteto.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa