Januari 26, 2026, Wilaya ya Kiteto imefanya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema Emmaniel ambapo katika kikao hicho ametoa maagizo kwa watendaji wa vijiji kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa sheria katika maeneo yao.
“Usimamizi madhubuti wa sheria ni miongoni mwa njia muhimu za kuzuia na kutatua migogoro inayojitokeza katika jamii, hususan migogoro ya ardhi na matumizi ya rasilimali”, alisema Mhe. Mwema

Aidha, amewataka Maafisa Kilimo na Mifugo wa kata kuhakikisha wanaufahamu kwa kina mipango ya matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao ili kuwaelekeza wakulima na wafugaji kufanya shughuli zao katika maeneo sahihi, jambo litakalosaidia kupunguza migongano na kuongeza tija katika uzalishaji.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mwema alisisitiza umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya umma, akibainisha kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa majengo ya serikali, miundombinu ya maji, barabara na umeme. Ameeleza masikitiko yake kuona baadhi ya miundombinu hiyo ikiharibiwa na wananchi, na kuwaagiza watendaji kuhakikisha sheria zinasimamiwa ipasavyo ili kulinda miundombinu hiyo.

Kikao hicho pia kilipokea uwasilishaji wa rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na taasisi mbalimbali za serikali zikiwemo TARURA, RUWASA, KIUWASA na TANESCO. Mbali na bajeti, taasisi hizo ziliwasilisha pia taarifa za utekelezaji wa miradi katika bajeti iliyopita.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa