Kuanzia kushoto ni mwakilishi wa Shirika la Copa Cocacola Bw.Omary Sudi katikati ni Afisa Michezo wa Wilaya Bi. Juliana Mtei na kulia ni Bw. Fabia Simon ambaye alipokea vifaa husika kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto leo tarehe 13.08.2019
Bw. Fabian Simon kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji (W) kulia akikabidhiwa baadhi ya vifaa hivyo na Bw. Omary Sudi kushoto katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
Picha mbalimbali za waalimu wa Shule za Sekondari husika waliokuwa wakipokea vfaa hivyo na Bw. Omary Sudi kushoto katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
------------------------------------ HABARI KWA UFUPI --------------------------------
Wafadhili wa Shirika la COPA COCALOLA linalofanya kazi pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wametoa msaada wa vifaa vya michezo ambavyo ni Jezi 32, Mipira ya Mpira wa miguu 7 na Mipira ya mpira wa kikapu 7, vifaa vyote hivi vina thamani ya Shilingi 3,220,000/=. Shule saba za Sekondari zilizopata vifaa hivi ni Sunya, Kibaya, Kiteto, Njoro, Dongo, Lesoit na Ndedo zote hizi ni Sekondari za Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Lengo kuu la kutoa vifaa hivi ni kuongeza tija katika michezo kuanzia ngazi za chini zikiwemo shule za Sekondari ili kuchochea vipaji vya wachezaji wa mpira nchini.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bw. F.Simon ameshukuru sana kwa Shirika hilo la COPA COCACOLA kwa kuipendelea Halmashauri yake kupata vifaa hivi na ameahidi Maafisa na Waalimu husika wanaoshugulikia michezo kutumia vifaa hivyo vizuri na weledi wa hali ya juu ili kuibua vipaji kwa wanafunzi wetu kwa lengo zima la kukuza soka si tu kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto bali na Taifa la Tanzana kwa ujumla wake. Hata hivyo tukumbuke kuwa michezo ni kuendeleza afya bora, Michezo ni ajira na kukuza uchumi kwa sekta mbalimbali ambazo ni mtambuka.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa