Hatimaye Wananchi wa Kijiji cha Ndirigishi, Wilaya ya Kiteto wamepata neema katika huduma za Afya baada ya Serikali kuwajengea Zahanati katika Kijiji chao na hivyo kuwaondolea adha ya kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 42 hadi Kibaya kufuata huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya.
Zahanati hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 87 imefunguliwa rasmi Agosti 29, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kushuhudia ufunguzi huo.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye ufunguzi wa Zahanati hiyo Mhe. Mwema aliwaeleza kuwa Serikali ya Awamu ya sita ina dhamira thabiti ya kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi kwa ukaribu zaidi ili kuwaepusha na usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufuata huduma.
Sambamba na hayo Mhe. Mwema aliwasihi wananchi hao kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa zanahati hiyo kwani wamepelekwa pale kuwahudumia.
Kukamilika kwa zahanati hiyo kutasaidia kupunguza vifo vya uzazi, watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano, pamoja na kuimarisha huduma za chanjo kwa watoto na wajawazito.
Zahanati ya Ndirigishi pia inatarajiwa kuhudumia vijiji jirani, na hivyo kuwa mwanga mpya wa matumaini kwa mamia ya wananchi waliokuwa wakihangaika kwa muda mrefu kufuata huduma za afya katika maeneo ya mbali.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa