Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema, Agosti 29, 2025, alifungua rasmi Zahanati ya Engusero Sidan ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 51, hatua inayotafsiriwa na wananchi kama ushahidi wa utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhesiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi huo, Mhe. Mwema alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi hususan vijijini na kuwapunguzia adha ya wananchi hao wa Engusero Sidan waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.
“Uwepo wa zahanati hii ni alama ya Serikali inayojali wananchi wake, Serikali imedhamiria kuhakikisha kila Mtanzania hata aliye pembezoni anapata huduma bora za afya mahali alipo badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo” alisema Mhe. Mwema ambaye alipokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa Engusero Sidan.
Wananchi waliokusanyika kwa furaha walimshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayeongoza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuona umuhimu wa afya zao haswa kwa upande wa Wanawake wajawazito ambao walikua wanalazimika kwenda umbali mrefu kwenda kujifungua.
Kwa mujibu wa taarifa ya mradi iliyosomwa mbele ya DC Mwema, Zahanati ya Engusero Sidan inatarajiwa kupunguza vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua, kuimarisha huduma za dharura na kuongeza matumaini mapya kwa jamii hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na changamoto za huduma za afya.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa