Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto, Ndg. Mufandii Msaghaa, amewataka wanaume kuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya msingi ya kunyonya maziwa ya mama, akisisitiza kuwa jukumu hilo si la mama pekee bali la familia nzima.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani yaliyofanyika Mbeli kijiji cha Kimana Agosti 7,2025, Ndg. Msaghaa alionya dhidi ya tabia ya akina baba kunyonya maziwa ya mama, akibainisha kuwa huwanyima watoto lishe stahiki.
Maziwa ya mama ni chakula bora kwa mtoto katika miezi sita ya mwanzo wa maisha, kwani yana virutubisho vyote muhimu, kinga dhidi ya maradhi, na huchangia katika ukuaji wa mwili na akili. Kunyonyesha husaidia pia kuimarisha uhusiano wa kipekee wa upendo kati ya mama na mtoto, pamoja na kumpa mama faida za kiafya, ikiwemo kupunguza hatari ya saratani ya matiti na ovari.
Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Duniani huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Agosti kote duniani ili kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kunyonyesha na kuhimiza ushirikiano wa familia, jamii na serikali katika kumsaidia mama kunyonyesha.
Maadhimisho ya hayo yalipambwa na burudani mbalimbali na elimu ya afya kutoka kwa wataalamu, huku kauli mbiu ikisisitiza kuweka mazingira wezeshi ya kumuwezesha mama kumnyonyesha mtoto wake.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa