Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akitoa maelekezo ya serikali katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Diwani wa kata ya Sunya Mhe. Mussa Brighton akiwasilisha taarifa ya kamati yake katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto kikiendelea.
..........HABARI KAMILI...........
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Magessa amewataka Waheshimiwa madiwani kushirikiana kuimarisha ulinzi katika maeneo yao ili kudhibiti utoroshwaji wa mazao unaotokea wakati wa mavuno, hali inayosababisha Halmashauri kupoteza mapato. Mhe. Magessa ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa maelekezo ya serikali katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Akizungumza wakati akitoa maelekezo hayo Mhe. Magessa amesema “Njia zinazopitishwa mazao zinajulikana,Kila diwani akisimama imara tutapata taarifa sahihi kuhusu mazao yanayosafirishwa.”
Mheshimiwa magessa amesema kwamba wakidhibiti vizuri, sulala la utoroshaji mazao lisipokuwepo watamsaidia Mkurugenzi , ambapo ataweza kujenga shule, kujenga zahanati na kufanya shughuli nyingine nyingi za maendeleo .
Akisisitiza kuhusu madhara ya halmashauri kukosa mapato Mhe. Magessa amesema “Kama hakuna pesa hapa itakuwa shida sana hapa,itakuwa ni ugomvi Jumatatu hadi Jumatatu.Halmshauri yetu inalindwa na mazao,tusiruhusu mazao yapite”.
Katika hatua nyingine Mhe Magessa amezungumzia masuala mbalimbali likiwemo maonyesho ya kilimo maarufu kama Nanenane na ujio wa mwenge wa uhuru na viwanda, ambapo katika suala la maonyesho ya Nanenane amewataka Wahe. madiwani kuhakikisha kwamba kila kata inatoa watu kwenda kwenye maonyesho, na sio tu kwenda kushiriki, bali wawe na vitu vya kwenda kuonyesha kwa lengo la kushindana.
Katika suala la ujio wa mwenge wa Uhuru , Mhe. Magessa amesisitiza kuhusu ushiriki wa wana Kiteto,ambapo amesema kwamba kila mtu ashiriki katika kufanya maandalizi ya mwenge kwani mwenge unaleta uhalisia wa nembo ya Taifa.
Aidha katika suala la viwanda Mheshimiwa Magessa amewataka madiwani kuhakikikisha kwamba kila mmoja katika kata yake kunakuwa na kiwanda kipya.
Katika kikao hicho ajenda mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na kusoma na kuthibitisha muktasari wa kikao kilichopita sambamba na kupokea na kujadili taarifa za kamati za kudumu.
....................MWISHO.....................
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa