• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DC Kiteto Apania Kuleta Mapinduzi ya Kilimo

Imetumwa : November 2nd, 2018

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akitoa maelekezo ya serikali ,katika siku ya pili ya  kikao cha baraza la madiwani Oktoba 31,2018, ndani ya ukumbi wa halmashauri .Waliokaa pembeni yake , upande wake wa kulia ni Mbunge wa jimbo la Kiteto Mhe. Emmanuel Papian, na upande wake wa kushoto ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Hassan Benzi.



.........HABARI KAMILI.......



Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Magessa amewataka Madiwani kulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo , ili wananchi wanaowaongoza waweze kuiga mfano kutoka kwao. Mhe. Magessa ameyasema hayo wakati akitoa maelekezo ya serikali katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto  Oktoba 31, 2018.


Akizungumza wakati akitoa maelekezo hayo Mhe. Magessa amesema kwamba kila diwani awe na mtaalamu wake mmoja ambaye atamuelekeza namna ya kulima kisasa , pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu katika shamba lake ,na kwamba agizo hilo ni lazima lianze kutekelezwa katika msimu ujao wa kilimo.Akisisitiza kuhusu agizo hilo Mheshimiwa Magessa amesema “ kila diwani alime kwa kufuata kanuni za kilimo bora, na mimi nitakuwa nikitembelea shamba la diwani mmoja baada ya mwingine. Naomba niwahakikishie kwamba nitafuatilia sana suala hili, tunataka tuone mabadiliko, ambayo yameanzishwa na sisi wenyewe,lazima tulime kilimo ambacho kitakuwa cha mfano kwa watu tunaowaongoza, na zaidi sana kilimo ambacho kitakuwa na tija kwetu”.


Kadhalika Mhe Magessa amewataka wakuu wa idara na wakuu wa vitengo wote, viongozi wa chama pamoja  na taasisi nyingine zote za serikali kufanya vivyo hivyo .Katika kuhakikisha kwamba ufuatiliaji wa utekelezaji wa agizo hilo unafanyika kikamilifu , Mheshimiwa Magessa amesema ‘‘najua kila mtu hapa ana shamba,wewe uliyejificha pori kwa pori kule ndani, mimi nitatembea tu,nitafika kote huko. Na ndugu zangu madaktari mjue, kama una shamba lima vizuri, fuata kanuni,waziri amesema ‘professionals’ wasikamatwe,sisi tutakukamata kwenye hoja ya shamba, sio ya udaktari.Kama umelima chini ya kiwango sisi hatutakuacha kwa sababu wewe ni daktari, tutakukamata tu kwa sababu ya kutotekeleza agizo hili la kwetu huku”.



Aidha Mheshimwa Magessa  amesema kwamba hata yeye mwenyewe  katika msimu ujao wa kilimo ana mpango wa kulima , na atalima kwa kufuata kanuni zote za kilimo bora. Mheshimiwa Magessa ameendelea kusema kwamba wao kama viongozi , wote wakifanya hivyo, na wakawaelekeza wanachi , na wananchi wakaelewa, na  kuiga mfano kutoka kwao, wakalima kisasa, wilaya ya Kiteto itafika mbali sana kiuchumi,kwa sababu  watavuna mavuno mengi ,watakuwa na chakula cha kutosha, na watakuwa na  chakula kingi zaidi cha kuuza, watapata fedha nyingi, na hivyo uchumi wa mwananchi mmoja mmoja utakuwa, uchumi wa wilaya pia utakuwa .


Wilaya ya Kiteto ni miongoni mwa wilaya ambazo  kilimo ni moja wapo ya shughuli kuu ya kiuchumi inayofanywa na wananchi wengi,lakini wengi wao, wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea, hawalimi kwa kufuata kanuni za kilimo bora, jambo ambalo linasababisha kilimo hicho kutokuwa na tija kwao, hali ya kuwa  wanalima maeneo makubwa,wanatumia nguvu nyingi, muda mwingi na fedha nyingi kulima,lakini mavuno yanayopatikana hayalingani na uwekezaji uliofanyika .




.................MWISHO......................



Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA: HATIMAYE KALOLENI YAPATA SHULE MPYA YA MSINGI

    July 30, 2025
  • SHULE YA MSINGI KINANGALI NAYO YANUFAIKA NA MRADI WA BOOST

    July 30, 2025
  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUWEKEZA KWA VITENDO: KURASH YAPATA MRADI MWINGINE WA MILIONI 153 KUPITIA BOOST

    July 30, 2025
  • KATA YA BWAWANI YAPATA MRADI WA SHULE MPYA YA ELIMU MSINGI.

    July 28, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa