Mgeni Rasmi (Mkuu wa Wilaya ya Kiteto) Mhe. Tumaini Magessa Akifungua Zoezi la Utoaji Elimu kwa Wadau wa NHIF , katika Ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya - Kiteto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona Akimkaribisha Mgeni Rasmi ( Mkuu wa Wilaya ya Kiteto ) Kufungua Zoezi la Utoaji Elimu kwa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kata kwa Kata , Katika Ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya - Kiteto.
Katibu Tawala Wilaya ya Kiteto Ndg. Stephano Ndaki akisililiza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Utoaji Elimu kwa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kata kwa Kata , Uliofanyika Katika Ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya - Kiteto.
Afisa Utumishi ( W) ya Kiteto Ndg. Laurent Kimaro ( aliyekaa upande wa Kushoto) na Mganga Mkuu ( W) Kiteto Malkiadi Paschal Mbota ( Aliye kaa upande wa Kulia) wakisililiza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Utoaji Elimu kwa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kata kwa Kata, Uliofanyika Katika Ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya - Kiteto.
Kaimu Meneja wa NHIF Mkoa wa Manyara Ndugu Yosia Mjema Akizungumza baada ya Ufunguzi wa Zoezi la Utoaji Elimu kwa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kata kwa Kata , Uliofanyika Katika Ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya - Kiteto.
Kaimu Meneja wa NHIF Mkoa wa Manyara Ndugu Yosia Mjema Akiweka Kumbukumbu ya Maswali na Changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Baada ya Kupewa Elimu na Maafisa wa NHIF Katika Ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya ,Ikiwa ni Mwanzo wa Zoezi la Utoaji wa Elimu kwa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kata kwa Kata Wilayani Kiteto.
Afisa Wanachama wa NHIF Mkoa wa Manyara Ndugu Charles Nyaurago Akitoa Elimu kwa Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto , Katika Ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya - Kiteto.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Wakifuatilia kwa makini Elimu iliyokuwa ikitolewa na Maafisa wa NHIF Mkoa wa Manyara , Katika Ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya - Kiteto.
................HABARI KAMILI.................
DC Kiteto Awataka NHIF Kuondoa Urasimu katika Taratibu za Utoaji Mikopo ya Miradi ya Ujenzi.
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Magessa ameutaka uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) kuondoa urasimu katika taratibu za utoaji mikopo ya miradi ya ujenzi ili kuziwezesha halmashauri na taasisi nyingine za serikali kuweza kuchukua mikopo kwani, kwa sasa pesa nyingi katika mikopo hiyo hutumika katika kugharamia mambo mbalimbali ambayo ni sehemu ya taratibu za kupata mikopo hiyo, hali inasababisha kutoonekana kwa thamani halisi ya fedha (value for money) katika miradi inayotekelezwa kwa fedha za mikopo . Mhe. Magessa ameyasema hayo alipokuwa akifungua zoezi la utoaji elimu kwa wadau wa bima ya afya kata kwa kata uliofanyika katika ukumbi wa kituo cha jamii ( Community Center) kilichopo katika mji mdogo wa Kibaya wilayani Kiteto.
Akizungumza katika ufunguzi huo Mheshimiwa Magessa anasema “ ndani ya NHIF kuna urasimu ule wa zamani,ili kukidhi vigezo vya kupata mkopo wa ujenzi unahitaji mshauri ( Consultancy) unahitaji hiki,unahitaji kile halafu baadae ndio hiyo hela ya mradi itoke.Serikali imekwisha hama huko,iko kwenye force account.Tukisema sisi tuna shilingi 200,000,000/= halafu tukaenda kwa utaratibu wa zamani ,mshauri anataka pesa, sasa tukija kulinganisha ule mradi tulioufanyia kazi na pesa tuliyotumia kwa kufuata taratibu zenu ,akaja mtu,kwa mfano mkuu wa mkoa,tunasema kwamba huu ndio mradi ulifadhiliwa na NHIF ,shilingi ngapi? 200,000,000/= atakachosema ni kwamba thamani ya fedha ina shida hapa.Thamani ya fedha haipo.Itarushwa kwenye vyombo vya habari,itaonekana kama mkurugenzi na viongozi wengine wamekula fedha.Hadi wajieleze ieleweke kwamba ni taratibu zenu ndizo zimesababisha gharama imefika kiasi hicho,majina ya watu yameshachafuka kiasi ambacho itachukua muda mrefu kuyasafisha.Ndio sababu halmashauri inakuwa na hali ya kusitasita katika kukamilisha taratibu za upatikanaji wa mikopo hii.Fikirieni ni namna gani mtaondoa taratibu hizi zinazoongeza gharama ili tuweze kuchukua mikopo tukarabati majengo ya hospitali ,tujenge wodi na miradi mingine’’.
Aidha Mhe. Magessa amesema kwamba zoezi hilo la utoaji elimu ni muhimu sana katika kuwawezesha wadau kufahamu mafanikio na changamoto zinazoukabili mfuko katika kutimiza majukumu yake na wajibu wa wanachama kama wadau katika kuhakikisha kwamba pande zote zinafanikiwa na kila upande unatimiza wajibu wake.Kuwapa fursa wadau na uongozi kujadiliana kwa uwazi jinsi ya kuboresha huduma za mfuko na kutimiza wajibu. Hivyo washiriki pamoja na uongozi wa NHIF wadumishe utaratibu wa majadiliano kwani ndio njia pekee itakayowezesha kupata ufumbuzi wa changamoto. Vilevile kupata elimu na uelewa wa kutosha kuhusu mambo muhimu yanayohusu mfuko.Vilevile Mhe. Magessa amewaeleza washiriki kwamba ni vema wakatumia fursa hiyo kuwasilisha kero zote wanazokutana nazo , kwani ndio mahali sahihi pa kuzungumza mambo yote, badala ya kulalamika mitaani . Kulalamika mitaani ni kelele kwa sababu sio mahali sahihi pa kupata majibu ya kero zao.
Vilevile Mhe. Magessa ametoa wito kwa washiriki wa zoezi hilo kuwaelimisha wengine ,Mhe. Magessa amesema kwamba kila mdau aliyepata elimu hiyo akiwa na uwezo wa kuelimisha watu 10,elimu hiyo itaweza kuwafikia watu zaidi ya 400.Hapa Mhe. Magessa anasisitiza anasema ‘‘Wewe uliyekuja hapa leo unatakiwa ukawaelimishe watu wengine yale ambayo mtajifunza na ambayo mtajadiliana hapa.Kawashirikishe elimu hii watu wengine ambao ni wanachama wa mfuko ili nao wapate uelewa ,wajue jinsi watakavyokabiliana na changamoto watakazokutana nazo katika huduma za matibabu zinazohusu bima ya afya.
Katika hatua nyingine Mheshimwa Magesa ametoa maagizo kuhusu utekelezaji wa shughuli za NHIF NA ICHF wilayani Kiteto ambapo amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ya Kiteto daktari Malkiad Paschal Mbota kukusanya taarifa zinazohusu utekelezaji wa shughuli za NHIF na ICHF kwa waganga wafawidhi wa zahanati na vituo vyote vya afya na kuwasilisha taarifa hizo kwake. Vilevile amemuagiza afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kuweka utaratibu wa kujadili utekelezaji wa huduma za bima ya afya katika sekretarieti ya huduma za jamii.Pia ameutaka uongozi wa NHIF Manyara kuweka utaratibu wa kumpatia taarifa kila baada ya miezi mitatu zinazohusu wilaya ya Kiteto kama vile idadi ya wanachama,changamoto wanazokutana nazo ili kwa kushirikiana waweze kuzifanyia kazi na kuhamasisha jamii kujiunga na bima ya afya. Kwa sababu wananchi wanapokuwa na bima za afya wanakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wote,jambo ambalo litaimarisha afya zao na wanapokuwa na afya njema uchumi wao pia utaimarika .
Akizungumza baada ya ufunguzi wa zoezi hilo la utoaji elimu kwa wadau wa NHIF kaimu Meneja wa NHIF mkoa wa Manyara ndugu Yosia Grayson Mjema anasema ‘‘inawezekana ninyi huko mnakopata huduma za matibabu mmekuwa mkikutana na changamoto mbalimbali ambazo leo hii tumekuja kuzisikiliza ,yale tutakayoweza kuyajibu hapa tutayajibu,yale ambayo yatakuwa yanahitaji msisitizo wa menejimenti tutayachukua na kuyapeleka kwenye menejimenti ili waweze kuyafanyia kazi na kuyapatia ufumbuzi’’
Katika ufunguzi wa zoezi hilo kaimu meneja wa NHIF ndugu Mjema na afisa wanachama wa NHIF mkoa wa Manyara ndugu Charles Nyaurago wametoa elimu kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kuhusu utaratibu wa kujiunga na bima ya afya, aina za bima ya afya, nani wanastahili kuwa wategemezi wa mwanachama mchangiaji,huduma zinazotolewa na mfuko; kuanzia kumuona daktari , vipimo na dawa .Taratibu za kumuondoa mtegemezi aliyevuka umri wa utegemezi au aliyefariki,taratibu za kumuingiza mtegemezi mpya kwenye nafasi ya mtegemezi aliyefariki au kuvuka umri.Taratibu za kupata kadi nyingine ya NHIF baada ya kadi ya awali kupotea au kubadilisha kadi kutokana na kubadilika kwa muonekano wa mwanachama mwenye kadi husika.
Pia washiriki walipata nafasi ya kufanya majadiliano, vilevile kuwasilisha kero na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wanapokwenda kupata huduma za matibabu ,ambapo Maafisa hao wa NHIF waliweza kutoa majibu ya changamoto na kero hizo , na kuahidi kuzifikisha kwa uongozi zile ambazo hawakuweza kuzipatia majibu ya papo hapo. Sambamba na hayo walitoa namba zao za simu kwa washiriki hao ili waweze kuwasiliana nao na kupata msaada au ufafanuzi pindi watakapokutana na changamoto au jambo lolote lenye utata linalohusu bima ya afya .
..................... MWISHO .........................
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa