Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akikagua ujenzi wa shule katika kijiji cha Lergu wilayani Kiteto.Kushoto ni diwani wa kata ya Kijungu mhe. Mandaro Mussa
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akiwa katika harambee ya ujenzi wa shule katika kijiji cha Lergu wilayani Kiteto.Kulia ni diwani wa kata ya Kijungu mhe. Mandaro Mussa na watendaji wengine wa serikali waliombatana nae katika harambee hiyo.
Diwani wa kata ya Kijungu Mhe. Mandaro Mussa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lergu wilayani Kiteto kabla ya harambee ya ujenzi wa shule.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magesa.
Wakazi wa kijiji cha Lergu wilayani Kiteto wakiwa katika harambee ya ujenzi wa shule.
Hatua mbalimbali za ujenzi wa shule katika kijiji cha Lergu kama inavyoonekana katika picha
Habari kamili......
DC Kiteto Aendesha Harambee ya Ujenzi wa Shule katika kijiji cha Lergu
Mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa Tumaini Magesa ameendesha harambee ya ujenzi wa shule katika kijiji cha Lergu kata ya Kijungu wilayani Kiteto. Mheshimiwa Magessa amesema kwamba ni muhimu kila mwananchi wa eneo hilo kuchangia katika harambee hiyo kufanikisha ujenzi wa shule , ili kuwawezesha watoto wa kijiji hicho kuweza kupata elimu mara tu wanapofikia umri wa kuanza shule.
Akisisitiza kuhusu umuhimu wa elimu mheshimiwa Magessa anasema ‘‘Mimi tangu niliporipoti hapa nilisema kazi yangu ya kwanza ni elimu .Tukiwa na elimu , hata migogoro itapungua. Hii ni awamu ya tano ndugu zangu, muda wa kusemasema umekwisha, ni muda wa kufanya kazi tu, shule iwepo hapa. Fedha ya kujenga madarasa mawili ipatikane leo hapa.Wafugaji ninaowaona hapa nina amini hakuna mwenye ngombe wawili ,kila mmoja ana ng’ombe wengi, lakini kijiji hakina shule. Kila mmoja ajisikie kwamba anawajibu wa kuhakikisha kuwa kijiji hiki kina kuwa na shule ili watoto wetu waweze kupata elimu bila kutembea umbali mrefu.Tutumie rasilimali tulizo nazo tuweze kukamilisha ujenzi wa shule’’.
Aidha mkuu wa wilaya amesema kwamba watu wa kijiji hicho wengi hawajui kusoma na kuandika , si kwamba hawakupenda kwenda shule , isipokuwa mazingira hayakuwaruhusu kwenda shule kutokana na kutokuwepo kwa shule katika kijiji hicho tangu mwaka 1993, ambapo shule iko umbali wa kilomita 30 kutoka kijijini hapo.Na kwamba imefika wakati sasa kijiji hicho na kijiji cha Ngapapa ambacho pia hakina shule , kuwa na shule ili kuondokana na hali hiyo ya kutokujua kusoma na kuandika.
Mheshimiwa Magessa amewataka wananchi wa vijiji vya Lergu na Ngapapa kuhakikisha kwamba ifikapo Disemba mwaka huu, vijiji hivyo vinakuwa na shule .Katika harambee hiyo kiasi cha shilingi milioni 4.9 ziliahidiwa ,ambapo mheshimiwa Magessa amechangia kiasi cha shilingi 1000,000.Fedha zote hizo zitakusanywa katika wiki moja ili kuwezesha ujenzi wa madarasa kuendelea.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa