Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema, amepongeza maandalizi ya Maonesho ya Nanenane kwa mwaka huu, huku akieleza kuwa amefurahishwa na mabadiliko yaliyofanyika ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Pongezi hizo amezitoa Agost 6, 2025 kwa Kamati ya Maandalizi mara baada ya kumaliza kukagua baadhi ya mabanda kwenye maanesho hayo akiwa kama Mgeni Rasmi wa siku hiyo.
Mhe. Mwema aliishauri Kamati hiyo kuyafanyia kazi maoni ya Wakuu wa Wilaya ambayo huyatoa mara baada ya kumaliza ziara za kukagua mabanda kwani maoni hayo yana tija kwenye kuyaboresha maonesho.
Aidha ameiambia Kamati hiyo kuona umuhmu wa kufanya tathmini kila maonesho yanapoisha na kwa kufanya hiyo itasaidia kuboresha zaidi maonesho ya miaka ijayo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa