Agosti 1,2024 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema aliongoza Kikao Cha Tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 wilayani hapo.
Kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Mwenge wa Uhuru kililenga kujua mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa maandalizi na siku husika ya Mwenge wa Uhuru ulipokimbizwa wilayani hapo.
Awali Mratibu wa Mbio za Mwenge Wilayani Kiteto, Ndug. Rodrick Kidenya alitoa taarifa za ujumla za kuanzia maandalizi ya mapokezi ya Mwenge, taarifa ya siku husika ya Mwenge wa Uhuru kuwepo Wilayani hapo na taarifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Simanjiro.
Wenyeviti wote wa kamati mbalimbali za Maandalizi ya Mbio za Mwenge 2024, walipata fursa ya kutoa taarifa ya matumizi ya kamati zao , kueleza majukumu waliyotekeleza na kueleza changamoto walizokutana nazo. Aidha wajumbe mbalimbali walipewa nafasi kuchangia taarifa zilizotolewa na wenyeviti wa kamati hizo.
Mhe. Mwema alisema kwamba, kikao hicho kilikua muhimu kwani kitasaidia kuboresha Maandalizi ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwa miaka ijayo.
Aidha Mhe. Mwema ametoa shukrani kwa Chama Cha Mapinduzi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, wanakamati, wananchi, taasisi binafsi na za serikali na watumishi wote kwa ushirikiano wao waliounesha toka wakati wa maandalizi hadi kukamilika kwa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Wilaya hapo.
Katika kikao hicho aidha Mhe. Mwema aliweza kukata keki iliyoandaliwa na mmoja wa wanakamati hao, na kuwalisha wajumbe wote ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwashukuru kwa kuweza kufanikisha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024.
Mwenge wa Uhuru Wilaya hapo ulipokelewa Julai 17, 2024 na kukimbizwa umbali wa takribani kilomita68 na kuzindua, kufungua na kutembelea miradi yenye jumla ya thamani ya TZS Bilioni 3.37. Mwenge wa Uhuru uliridhia miradi yote wilayani hapo.
“Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mtaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa