Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Remidius Mwema Emmanuel, ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Magungu –Nhati wenye thamani ya shilingi 1.2bil. uliopo katika kata ya Magungu.
Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, Kaimu Mkurugenzi pamoja na wananchi, limefanyika Machi 21, 2024 kwenye kijiji cha Magungu katika Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kiwilaya.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa RUWASA Kiteto, Mhandisi Stephano, Mbaruku, amesema kwamba Mradi wa Maji Magungu-Nhati uliibuliwa na RUWASA kwa kushirikiana na jamii na Halmashauri ya Wilaya Kiteto. Mwaka 2022/2023 RUWASA ilipokea fedha kutoka serikali kuu kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao kisima chake kina urefu wa mita 120 na kwasasa kina uwezo wa kuzalisha maji lita 26,000 kwa saa.
“Mradi wa Maji Magungu –Nhati umetelezwa kwakutumia wataalamu wa ndani kuanzia 15 Septemba 2022 na kakamilika 30/7/2023 na kwasasa utekelezaji wa mradi huu umekalika kwa asilimia 100,” aliongeza Mhandisi Mbaruku.
Akiongea katika hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwe la Msingi na Maadhimisho ya Wiki ya Maji, Mgeni Rasmi Mh.Mwema aliishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za mradi huo na pia aliipongeza jamii na RUWASA kwa kutekeleza mradi huo.
Aidha Mh. Mwema alikemea vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya maji ambao umekua ukifanywa na baadhi ya wananchi kwenye baadhi ya maeneo na kufanya jamii kukosa huduma ya maji na kuipa serikali hasara.
Mbali na hayo, Mh. Mwema amekataza shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji na kuagiza utunzaji wa mazingira kwenye vyanzo vya maji.
“Lazma vyanzo vya maji vitunzwe maeneo yote yenye vyanzo vya maji, miti ipandwe”, aliongeza Mh. Mwema.
Mradi wa Maji Magungu- Nhati utahudumia zaidi ya wakazi 7,500 wa kijiji cha Magungu na Nhati. Kukamilika na kuanza kazi kwa mradi huu kunawaongezea wananchi wa vijiji hivyo muda wa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji. Aidha kunapunguza magonjwa yatokanayo na ukosefiu wa maji safi na salama.
Kata ya Magungu ina vijiji vitatu ambavyo ni Magungu, Nhati na Emarti ila kwasasa mradi huo unahudumia kijiji cha Nhati na Magungu. Hivyo DC Mwema amewaambia RUWASA kuangalia namna ya kuwawezesha wanakijiji wa Emarti nao wananufaika na mradi huo.
Katika kutekeleza mradi huo, jamii ilichangia kiasi cha sh 2m, Chombo cha Watumia Maji 37M na serikali kuu 1.2bil.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa