Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bi. Dora Mziray, ametoa rai kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kuhakikisha hawawi kikwazo katika ukusanyaji wa mapato, akisisitiza kuwa usimamizi wao ndiyo msingi wa kuinyanyua Halmashauri kiuchumi na kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Akizungumza katika Mkutano wa Kwanza wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Desemba 02, 2025, Bi. Dora amesema madiwani wana jukumu kubwa la kusimamia matumizi sahihi ya fedha, kushiriki katika uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato, na kuhakikisha hakuna vitendo vinavyokwamisha makusanyo ya Halmashauri.
Aidha, Bi. Dora aliwasihi madiwani hao kushirikiana na viongozi na wataalumu ili kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa wilayani hapa inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Awali, Mwenyekiti wa Muda wa kikao hicho, Ndugu.Mufandii Msaghaa, wakati akifungua Mkutano huo, aliwataka madiwani kutimiza ahadi walizowapa wananchi wakati wa kampeni na kuwatumikia kwa weledi.

Vilevile aliwahimiza madiwani hao kusoma na kufahamu miongozo ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.
Ndugu Msaghaa amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya madiwani, wataalamu na viongozi wengine ni msingi muhimu wa kufanya baraza kuwa na nguvu na uwezo wa kupanua wigo wa mapato ya Halmashauri.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa