Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona akisalimiana na wachezaji wakati akikagua timu tayari kwa kuanza UMISETA ngazi ya wilaya.Walio nyuma yake ni Afisa elimu Sekondari (W) Ndg. Mtinga Maleya na Mratibu wa UMISETA (W) Ndg. Riziki Lymo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa UMISETA wakati akifungua UMISETA ngazi ya wilaya.
Timu zikiwa zimejipanga tayari kuanza UMISETA ngazi ya wilaya.
..............HABARI KAMILI............
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona,amewataka wanafunzi wanaoshiriki katika Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania ( UMISETA ) ngazi ya wilaya kuonyesha jitihada ili waweze kufuzu vigezo vya kushiriki katika michezo hiyo kimkoa na hata kitaifa.Ndugu Kambona ameyasema hayo wakati akifungua kambi michezo hiyo, ambapo watapatikana washiriki watakaoiwakilisha wilaya katika UMISETA mkoani.
Akisisitiza kuhusu washiriki washiriki hao kufanya bidii katika michezo hiyo, Kambona amesema “Mimi mkurugenzi kwa nafasi yangu nitaonyesha jitihada,kuhakikisha kwamba mnapata kila mnachotakiwa kupata wakati wote mtakaokuwepo katika michezo hii,walimu kwa nafasi yao wataonyesha jitihada zao.Tunataka tuone mkifanya jitihada.Ni jitihada pekee itakayowawezesha kufika mbali katika michezo hii.Mtafika babati mkoani, mtafika Mwanza kwenye mashindano ya kitaifa,endapo tu mtaonyesha jitihada”.
Aidha ndugu Kambona amesisitiza kuhusu suala la nidhamu kwa washiriki wa michezo hiyo, ambapo amesema kwamba,kama ambavyo wamekuwa wakionyesha nidhamu wakati wakiwa mashuleni kwao,vivyo hiyo waonyeshe nidhamu hiyo wakati wote watakapokuwa katika michezo hiyo kambini hapo,na kwingine kote watakako kwenda katika michezo hiyo.Na sio kwamba waende wakafanye mambo ambayo ni kinyume na lengo lililokusudiwa.
Michezo hiyo itahitimishwa siku ya Ijumaa, washiriki waliochaguliwa kuwakilisha wilaya ngazi ya mkoa ,wataondoka siku hiyo hiyo ya ijumaa kuelekea makao makuu ya mkoa wa manyara ( Babati) .Huko UMISETA itaendelea ,ambapo watapatikana washiriki watakao wakilisha mkoa wa Manyara katika ngazi ya taifa ambayo hiyo itafanyika mkoani Mwanza.
..........MWISHO...........
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa